Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Showing posts with label kitaifa. Show all posts

WAZIRI PROF. MAGHEMBE AJIUZULU; DAWASA/DAWASCO WAREJESHA HUDUMA NDANI YA WIKI MOJA KATIKA MAENEO YALIYOKUWA YAKIPATA MGAWO WA MAJI KABLA

CHADEMADirectorofInformationandUbungolegislatorJohnMnyika1
Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA) Mh. John Mnyika.
Nimemtumia ujumbe Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe kumshauri ajiuzulu kutokana na kujirudia rudia kwa matatizo ya maji katika Jiji la Dar Es Salaam kinyume na maelezo yake ya uongo  aliyoyatoa bungeni tarehe 4 Februari 2013.
Aidha, Wenyeviti wa Bodi na Watendaji wakuu wa Mamlaka zinazohusika na huduma ya maji jijini (DAWASA na DAWASCO) watoe maelezo kwa umma juu ya sababu za kweli za matatizo ya maji kujirudia rudia katika Jiji la Dar Es Salaam.
Pia, wajieleze kwa umma ni kwanini wananchi wasipendekeze Rais awachukulie kwa uzembe, kuisababishia hasara Serikali, kuathiri  uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa kukosa maji mara kwa mara ambayo ni huduma ya msingi ya binadamu na malighafi muhimu katika uzalishaji.
Itakumbukwa kwamba tarehe 4 Februari 2013 niliwasilisha hoja binafsi bungeni juu ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji katika jiji la Dar Es Salaam, nikipendekeza Bunge kuingilia kati kuweza kuisimamia Serikali kuchukua hatua za haraka.
Iwapo hoja hiyo ingejadiliwa na maazimio yote kutekelezwa matatizo ya maji katika Jiji la Dar Es Salaam mpaka hatua ya sasa yangekuwa yamepungua katika maeneo mbalimbali kutokana na hatua ambazo nilipendekeza zichukuliwe.
Hata hivyo, badala ya kuunga mkono hoja hiyo ambayo ingeisaidia Wizara yake  na kurekebisha udhaifu uliokuwepo na hivyo kumrejeshea imani kwa umma ambavyo ilikuwa imepungua; Waziri Maghembe akaamua kinyume cha kanuni za Bunge kutoa hoja ya kuondoa hoja niliyowasilisha.
Katika hatua hiyo nilijaribu kutumia kanuni za Bunge kuweza kutoa ufafanuzi juu ya uongo wa Waziri Prof. Maghembe na hatua ambazo Bunge lilipaswa kuchukua. Hata hivyo Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai aliamua kukiuka kanuni kumlinda hali ambayo ilichochea vurugu bungeni.
Mara baada ya kurejea bungeni tarehe 10 Februari 2013 nilihutubia wananchi na kuwaeleza kusudio la kuandaa maaandamano kwenda Wizara ya Maji iwapo katika kipindi cha ndani ya wiki mbili Waziri Prof. Maghembe asingejitokeza kutoa maelezo kwa umma kuhusu masuala yote ambayo alipaswa kuyajibu bungeni juu ya hatua za haraka zilizopaswa kuchukuliwa.
Ndani ya wiki hizo mbili Waziri Maghembe alijitokeza mara mbili kuzungumzia masuala ya maji Dar Es Salaam; kupitia mikutano ya CCM ikiwemo katika kata ya Goba jimboni Ubungo na katika mkutano wake na wafanyakazi DAWASA na DAWASCO tarehe 21 Februari 2013 na kueleza hatua za haraka ambazo angesimamia zichukuliwe.
Hata hivyo, baada ya wiki moja bila ya Waziri wa Maji na Wizara kwa ujumla kuonyesha  kwa matendo kuisimamia kwa karibu EWURA, DAWASA, DAWASCO na Manispaa ya Kinondoni kuchukua hatua za haraka ambazo nilizieleza kwenye hoja binafsi, niliamua kuchukua hatua zaidi.
Nilitangaza kuongoza maandamano ya wananchi tarehe 16 Machi 2013 kwenda Wizara ya Maji ili kupata majibu na kuisimamia Serikali kuchukua hatua za haraka. Hata hivyo maandamano hayo yalizuiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu zisizo za msingi na kuombwa kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Nilikata rufaa lakini toka wakati huo mpaka anaondelewa katika nafasi yake Waziri Dr Emmanuel Nchimbi alikwepa kuchukua hatua dhidi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela kwa kuvunja sheria, kusababisha hasara na kuwanyima haki ya msingi wananchi ya kufikisha ujumbe kwa Serikali.
Maandamano hayo yangefanyika na hatua kuchukuliwa matatizo yangepungua tofauti na ilivyo sasa, hivyo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima anapaswa kueleza umma lini rufaa hiyo itashughulikiwa maandamano yaweze kufanyika wananchi wapate majibu ya hatua za haraka nilizopendekeza ndani na nje ya Bunge.
Zaidi ya nusu mwaka umepita toka Waziri Prof. Maghembe atoe ahadi ambazo ameshindwa kusimamia utekelezaji wake na hivyo kupaswa kujiuzulu. Iwapo Waziri Prof. Maghembe hatajiuzulu nitaeleza hatua zaidi ambazo nitachukua.
Wakati hatua hizo zikisubiriwa, natoa mwito kwa DAWASA na DAWASCO kuhakikisha kwamba katika kipindi kisichozidi wiki moja huduma za maji zinarejea katika maeneo ambayo yalikuwa yakipata mgawo wa maji.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
10/01/2013

RC Manyara ajikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa

 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo, amejikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi wa wilaya ya Kiteto,  kumzomea na kumtaka aondoke na mkurugenzi wake wakati alipokutana nao kuzungumzia  mgogoro wa wakulima na wafugaji.

Hali hiyo ilijitokeza wakati mkulima,  Ramadhani Machaku, aliposimama kuuliza swali, lakini Mkurugenzi wa Wilaya ya Kiteto, Jane Mutagurwa, kumnyang’anya kipaza sauti na kumtaka aulize swali badala ya kutoa hotuba.


Katika swali lake Machaku, alishutumu uongozi wa wilaya kuwa umechangisha mamilioni ya fedha kwa wafugaji ili kuhakikisha wakulima wanaondoka na matokeo yake kule mashambani wanaishi kama maadui na kuuana kinyama.


Aidha alisema kuwa viongozi wamekuwa hawataki kuongea ukweli kuhusu jambo hilo na kudai kuwa hawataondoka katika eneo hilo hadi hapo serikali itakapowahakiki wafugaji ambao ndiyo waliowauzia maeneo.


Alimuomba Rais Jakaya Kikwete au Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati kutatua mgogoro huo kutokana na viongozi wa wilaya hiyo kuwagawa wananchi na kupindisha ukweli.


Hatua ya mkurugenzi huyo kumnyang’anya kipaza sauti, kiliwakasirisha wananchi hao, ambao walianza kuzomea  huku baadhi wakisusia na kuanza kuondoka  kwenye mkutano huo, wakitaka Mkuu wa mkoa aondoke na mkurugenzi wake.


Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kiteto, Foka Dinya, aliingilia kati na kuwataka wananchi hao kuacha vurugu.


 Awali  Mbwilo ambaye alitoa fursa kwa wananchi kuuliza maswali, alikiri kuwa mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Kiteto unasababishwa na viongozi wa wilaya hiyo na kuiagiza kamati ya ulinzi ya mkoa kukaa kuangalia tatizo ili wilaya hiyo iwe na amani.


“Mambo haya tangu mwanzo nayafahamu lakini bado tunayafanyia kazi lakini ni kwa nini watu wanakubali kuchangishwa fedha bila ya utaratibu wa serikali na bila kibali maalum sisi kama serikali tunalifuatilia haiwezekani michango ichangishwe kikabila,”alisema.


Alisema kuwa  serikali ya mkoa inatambua suala hilo la viongozi kuhusika na mgogoro huo.


Alisema kuwa tangu juzi amefanya ziara na kupokea malalamiko na taarifa kuwa viongozi wa wilaya walipokea rushwa ya madume ya ng’ombe kutoka kwa wafugaji ili wakulima waondolewe katika Hifadhi hiyo.


“Wananchi kweli mmegawanywa katika makundi na inawezekana ni sisi viongozi ndiyo tuliofanya hivi na matokeo yake wafugaji wanaona wana haki ya kukaa ndani ya hifadhi huku wakulima nao wanaona wamehujumiwa kwanini wafugaji wakubaliwe,” alisema Mbwilo.


Alisema kuwa mgogoro huo ulitokana na baadhi ya wakulima kuingia katika eneo la hifadhi kinyume na sheria na kujichukulia ardhi kubwa mpaka kumiliki hekari 6000.


Aliwataka wakulima na wafugaji kuondoka katika hifadhi hiyo mpaka hapo watakapofanya utaratibu wa kugawa tena kulingana na vielelezo  watakavyowasilisha kuwa walipewa idhini na nani ya kumiliki maeneo hayo.


Aliwaagiza viongozi wa wilaya kuwaondoa katika eneo hilo wakulima na wafugaji wote kwa pamoja kwa kuwa wameingia kinyume na sheria tofauti na agizo la awali ambalo liliwataka wakulima kuondoka.


Awali mmoja wa wafugaji wa jamii ya Kimasai, Kisioki Masiyai, alisema kuwa chanzo cha mgogoro na kusababisha mapigano ni Mkurugenzi wa wilaya hiyo, ambaye aliwachangisha fedha wafugaji ili kuwaondoa wakulima.



Alisema kuwa hawatakubali kuondoka katika hifadhi hiyo mpaka hapo serikali ya wilaya hiyo itakapotoa mchanganuo wa matumizi ya mamilioni ya fedha ambazo walichangishwa wafugaji.
 

CHANZO: NIPASHE

NAOMI CAMPLE ATUAKENYA KWA AJILI HII...SOMA HAPA

Super model  Naomi Campell ameonekana  huko Pwani ya kenya. Kwasasa Kenya inahali nzuri ya hewa na macelebs wengi hupenda kuja majira haya kwa ajili ya mapumziko.Model Huyu mwenye umri wa miaka 43 si kwamba yupo kwa ajili ya mapumziko tu bali ameamua kujumlisha mapumziko yake na shughuli zake zakihumanitarian kusaidia watoto yatima nchini kenya.
naomi campell
naomi-malindi
Naomi alikua Nchini Kenya tokea mwishoni mwa mwaka 2013 na aliweza kukutana na watu wengine maarufu huko pwani ya malindi kama Flavio Briatore,63  ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini italia ambaye naye alikua mapumzikoni kwenye pwani hizo za malindi.
Naomi-Flavio-Briatore

PICHA ZA FAMILIA YA JAJI LAN MBUGUA WA TUSKER PROJECT FAME...ANGALIA PICHA HAPA

553698_10151049689310266_1105956410_n
Judge Ian Mbugua has always been known to be a no nonsense man especially in the last six episode of Tusker Project Fame that he has served as a Judge. Many love him, many fear him and many also
hate him but he does not seam to care much, as long as he expresses his opinion and does his work as is expected of him, people will talk and talk but he will remain to be who is.
ian2
Apart from the other things that this no nonsense Judge is known for, he has another side of his life. He is a family man. A loving father to three very beautiful, youthful kids and a loving husband to one wife. Below are some amazing pictures of this amazing family.
ian4 ian3 ian1
Source: http://niaje.com

ZITTO ASHINDAKESI DHIDI YA CHADEMA MAHAKAMA KUU...MATUKIO KATIKA PICHA

Zitto Kabwe akipeana mikono na Wakili wa CHADEMA,Tundu Lisu baada ya kukibwaga chake chake.
 Wakili wa chama cha CHADEMA,Mh Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar Es Salam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama chake.
 Tundu Lisu akiwatuliza na  kuwasihi wafuasi wa chama chake CHADEMA kutokufanya fujo na badala yake waondoke eneo hilo kwa utulivu na amani.Nje Mahakama makundi ya wafuasi wa CHADEMA na Zitto Kabwe walikuwa wakirushiana mawe kiasi hata mmoja wa wafuasi wa CHADEMA kujeruhiwa kichwani kwa jiwe.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amekibwaga chama chake,kufuatia  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.

Aidha Wakili wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na maamuziki ya Mahakama,hivyo akabanisha kuwa  Zitto Kabwe atabaki kuwa Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una  muda wake basi tujipe muda tuu..alibainisha Tundu Lisu.

TAARIFA JUU YA MWANAMKE ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DARESALAAM HAPO JANA AKIPELEKA NCHINI CHINA

Mwanamke mmoja  Salma Omari Mzale, alikamatwa Airport Dar es Salaam na Madawa ya Kulevya, akielekea nchini China. Mpaka sasa ameshikiliwa na Polisi wa usalama kitengo cha madawa ya kulevya cha uwanja wa ndege. Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege. Hadi saa 1 jioni (mida ya Tanzania). Uchunguzi wa kina unaendelea.
Habari kamili itawajia hivi punde.

TAMKO LA NIMROD MKONO KUHUSU KUMUHONGA GARI 2 ZITTO KABWE


MH. MKONO KUMPATIA MH. ZITTO MAGARI MAWILI


Nimesikitishwa na jinsi Chama kikuu cha upinzani ambavyo kwa siku za hivi karibuni kimeingia katika migogoro ambayo inaathari kubwa kwa ustawi wa demokrasia hapa nchini.
Nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mimi Mh. (Nimrod Mkono) kumpatia Zitto Kabwe (MB) magari mawili (Land Cruiser pamoja na Nissan Patrol).
Kwanza napenda ifahamike kwamba sijawahi kumpatia Zitto magari. Isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser; nilitoa msaada wa kuwanusuru kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Zakayo Wangwe (MB) Tarime. Wakiwa wanatishiwa kupigwa (Freeman Mbowe pamoja na Zitto Kabwe) nilijitolea gari langu lenye bendera ya Bunge, liwachukuwe na kuwapeleka Mwanza wakiwa salama, na ilifanyika hivyo. 
Baada ya kufika Mwanza, Mhe. Zitto aliwasiliana na mimi, kuhusu ununuzi wa gari hilo, nami kupitia kwa wakala wangu Africariers; nilimuuzia Zitto hilo gari.

Kuhusu hilo gari la pili: (Nissan patrol) Mhe. Zitto Kabwe alilikodi, na mpaka sasa anaendelea kulipa vizuri tu; lakini pia ifahamike kwamba hata nyaraka za gari hilo bado ninazo mimi kama mmiliki halali na sijawahi kuhamisha umiliki wake (Transfer of ownership)

KUHUSU KUTOA FEDHA KWA CHADEMA
Nimesikitishwa na ninataka kuweka wazi kwamba, sijawahi kuongea na Tundu Lissu kama inavyodaiwa kwa masuala yoyote binafsi isipokuwa tukiwa kwenye kamati ya Katiba na Sheria. 
Ikumbukwe kwamba, nimepita bila kupingwa kwa vipindi vitatu mfululizo (2000, 2005 na 2010). Ni historia ya aina yake; lakini pia uchapakazi wangu kwenye jimbo la Musoma vijijini. Ushindi wangu wa kupita bila kupingwa kwa kiwango kikubwa umekuwa unatokana na bila shaka umahiri wangu kwa kufanya kazi za wananchi kwa kiwango kikubwa.

MFAHAMU DESIGNER MTANZANIA ALIYE MVALISHA BEYONCE KWENYE MOJA YA SHOWS ZAKE..

Anajulikana kwa jina la Christina Mhando ni designer makazi yake yaliyopo jijini london,ame-graduate Kent University with an honours degree, mwaka 2002. Baada ya masomo yake ,Mhando alipata experience yakufanya kazi na designers wakubwa wa nguo za kike ulaya.Na ujuzi huo aliopata,Mzaliwa huyo wa Tanzania aliweza kufungua Lebel yake mpya mwaka 2007 iitwayo CHICHI  jina lililokuwa aka yake toka utotoni. brand inayotengeneza nguo kwa kuchanganya vionyo mbalimbali vya ubunifu wenye asili ya mahali alipotokea designer huyo kwa  kama “Khanga”kitambaa kinachotumika na wanaweke wengi east africa kwa kujifunika.
Collection yake ya kwanza kutoka kampuni ya Chichika ilifanikiwa kuuzwa sana huko ulaya nakufanya aweze kuuza na kupata order mbali mbali za nguo,kupata interview mbalimbali na media kubwa sana ikiwemo Vogue huko italy,kitu kilichompa moyo kuendelea fufanya vizuri sana na kufanya kampuni yake hiyo izidi kukua.
chichiass13-8_crop
moja ya nguo aliyoi-design CHICHI
bey_in_chi
Beyonce akiwa kwenye Show ya Mrs Carter Tour akiwa amevalia vazi la Chichi.
Hivi karibuni alikuwa-featured kwenye Vogue Italia Talents in 2013, Jambo lililovutia watu ni ubunifu wake wa kutumia colour and print za East Africa kitu kinachofanya label ya Chichia iwe na nguo za kipekee kufanya kuvutiwa hata na celebrity mbalimbali,Akiwemo msanii maarufu Beyonce ambaye naye pia ni mvaaji wa nguo alizo design, Chichia is fastly becoming recognised as an international African brand ambayo ina- transform traditional East African textiles into stylish, contemporary and considered fashionable kwa ujumla.
chiara_11
chichia
Baadhi ya mavazi ya Christine Mhando

DKT. JOSE CHAMELEONE ATUA JIJI LA MWANZA KUANGUSHA SHOO LA UKWELI LEO CCM KIRUMBA


Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusiana na Tamasha lililopewa jina la 'Badilisha Concert' litakalofayika leo 24 dec 2013 katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo kama sehemu ya kuikaribisha sikukuu ya Christmass. Pembeni yake anaonekana meneja wake na mwisho kabisa kulia ni mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo Mr. James Njuu wa K Vant Gin.


Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na mmoja kati ya wasanii wa Jambo Squard mbele kidogo ni Dogo Dee na mwisho kabisa (kushoto) katika mstari ni mwanamuziki Bob Haisa ambao wamefika kumpa sapoti katika show ya Badilisha Concert itakayofanyika leo CCM Kirumba Mwanza. 
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na ndugu zake wasanii wa Tanzania waliofika leo kuzungumza na waandishi wa habari katika Hotel Gold Crest Mwanza.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Denis (kushoto) kutoka Silver Intertainment amesema kuwa kampuni yake imeamua kuweka kiwango kidogo cha kiingilio ili watu wote wa Kanda ya Ziwa waipate zawadi ya mwaka kushuhudia burudani kali.
"Zawadi nyingi huwekwa kwenye boxi lakini hii yaani mimi ni zawadi iliyo nje ya boxi maalum kwa wakazi wa Mwanza" pia Jose Chameleone anasema kuwa najivunia kuwa Mwanza mji ambao kwangu ni sawa na nyumbani.
Jose Chameleone amekwepa kulizungumzia suala lake la hivi majuzi kukumbatiana na mdogo wake Weasal na binamu yake Radio ile hali walikuwa kwenye bifu kali akisema yote yatafanyika lakini undugu utabaki pale pale akisita kuendelea kulizungumzia suala hilo kwa undani akisema hawezi kuzungumzia masuala ya familia nje ya familia anaheshimu utamaduni wa kiafrika.






Jose Chameleone akiwa na wasanii wa Tanzania kutoka kushoto ni Bob Haisa, King Houston, Chemeleone (mwenyewe) Dogo Dee, Chuse, na Jambo Squard team.
Jose Chameleone akiwa na wadhamini waliosimamia mzigo ukasimama.
Take two na wadhamini.
Jose akiwa na wanahabari wa Mwanza.

DKT. JOSE CHAMELEONE ATUA JIJI LA MWANZA KUANGUSHA SHOO LA UKWELI LEO CCM KIRUMBA


Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusiana na Tamasha lililopewa jina la 'Badilisha Concert' litakalofayika leo 24 dec 2013 katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo kama sehemu ya kuikaribisha sikukuu ya Christmass. Pembeni yake anaonekana meneja wake na mwisho kabisa kulia ni mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo Mr. James Njuu wa K Vant Gin.


Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na mmoja kati ya wasanii wa Jambo Squard mbele kidogo ni Dogo Dee na mwisho kabisa (kushoto) katika mstari ni mwanamuziki Bob Haisa ambao wamefika kumpa sapoti katika show ya Badilisha Concert itakayofanyika leo CCM Kirumba Mwanza. 
Mwanamuziki mahiri toka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisalimiana na ndugu zake wasanii wa Tanzania waliofika leo kuzungumza na waandishi wa habari katika Hotel Gold Crest Mwanza.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo Denis (kushoto) kutoka Silver Intertainment amesema kuwa kampuni yake imeamua kuweka kiwango kidogo cha kiingilio ili watu wote wa Kanda ya Ziwa waipate zawadi ya mwaka kushuhudia burudani kali.
"Zawadi nyingi huwekwa kwenye boxi lakini hii yaani mimi ni zawadi iliyo nje ya boxi maalum kwa wakazi wa Mwanza" pia Jose Chameleone anasema kuwa najivunia kuwa Mwanza mji ambao kwangu ni sawa na nyumbani.
Jose Chameleone amekwepa kulizungumzia suala lake la hivi majuzi kukumbatiana na mdogo wake Weasal na binamu yake Radio ile hali walikuwa kwenye bifu kali akisema yote yatafanyika lakini undugu utabaki pale pale akisita kuendelea kulizungumzia suala hilo kwa undani akisema hawezi kuzungumzia masuala ya familia nje ya familia anaheshimu utamaduni wa kiafrika.






Jose Chameleone akiwa na wasanii wa Tanzania kutoka kushoto ni Bob Haisa, King Houston, Chemeleone (mwenyewe) Dogo Dee, Chuse, na Jambo Squard team.
Jose Chameleone akiwa na wadhamini waliosimamia mzigo ukasimama.
Take two na wadhamini.
Jose akiwa na wanahabari wa Mwanza.

Mkakati mpya wa kumng'oa Mizengo Pinda....wabunge 26 watia saini fomu maalumu ya kutaka Bunge limng'oe



Baadhi ya wabunge wameanzisha mkakati wa kumwondoa madarakani, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kile wanachodai kuwa hawaridhishwi na utendaji wake serikalini. 
 
Hiyo ni dalili kwamba kung’oka kwa mawaziri wanne kutokana na matokeo ya ripoti ya utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili hakujamnusuru Pinda, kwani baadhi ya wabunge wanaendelea na msimamo kwamba naye ajiuzulu kwa kushindwa kuwasimamia wenzake.
 
Mawaziri waliong’oka baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wao kutokana na ripoti iliyowasilishwa na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ni Mawaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo na Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
 
Hatua hiyo ya Rais Kikwete inatafsiriwa na wengi kama njia ya kuwapoza wabunge na kumwokoa Pinda ambaye ikiwa atang’oka itamaanisha kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri.
 
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili jana zinasema wabunge 26 wametia saini fomu maalumu ya kutaka Bunge litumie mamlaka yake ya kikatiba kumng’oa Pinda kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.
 
Kwa mujibu wa Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu, endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.
 
Kwa mujibu wa Ibara hiyo, hoja ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu inapaswa kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote.
 
Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali alisema hili jana kuwa ukusanyaji saini za wabunge aliouanzisha Ijumaa jioni unakwenda vizuri.
 
“Kung’oka kwa mawaziri wale wanne inatosha kuthibitisha kuwa Pinda amepoteza uhalali wa kuwa Waziri Mkuu kutokana na kushindwa kuwasimamia walio chini yake,” alisema Machali.
 
“Rais tunaweza kumuacha, lakini Pinda ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali. Kama wapo mawaziri wameboronga ni wazi na yeye anaingia moja kwa moja katika hilo kapu,” alisema na kuongeza:
 
“Kama kweli tunataka taifa lisonge mbele kutoka hapa tulipo ni lazima tumuondoe Pinda…….. amekuwa mpole mno, mzito kufanya uamuzi na analea matatizo.”
 
Hata hivyo, alisema wabunge waliosaini fomu hiyo, wote wanatoka kambi ya upinzani na kusema wabunge wengi wa CCM aliowafuata kuwaomba watie saini wanaogopa au wanasita kufanya hivyo.

“Nataka niwaambie wabunge wa CCM hebu tusimame katika masilahi ya umma… Serikali inapofanya vibaya wanaoumia ni wananchi wetu bila kujali ni mwanachama wa chama gani,” alisema.
 
Pinda tayari amesema wazi kwamba yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake iwapo Rais Kikwete ataamua kumuondoa na kwamba hata Rais asipochukua hatua hiyo ni ruksa kwa wabunge kutumia mamlaka yao ya kikatiba ya kumuondoa kwa njia ya kura ya kutokuwa na imani naye.
 
Wabunge wengine
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola ambaye alikuwa mwiba kwa Pinda bungeni alisema: “Haya ni mambo ya ajabu sana, tutaendelea kubadilisha glasi lakini mvinyo ni uleule”.
 
Alisema uwajibikaji wa Serikali unaanzia kwa Waziri Mkuu na kusema anamuomba Rais atafakari ombi lake la kumfuta kazi Pinda.
 
“Tufike mahali tuambiane ukweli bila kumung’unya maneno kama kweli tunataka kuisaidia nchi yetu na Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi ambayo inapendwa na kuaminiwa na Watanzania,” alisema Lugola.
 
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa  alisema anavyomuona Pinda na kutafsiri utendaji wake, anadhani kuwa viatu vya uwaziri mkuu vinampwaya.
 
“Haiwezekani mara mbili ndani ya Bunge mawaziri wang’oke halafu wewe ubaki… wanapoboronga katika utendaji wao lazima pia umguse kiranja wao (Pinda) na hili bado tutalia nalo,” alisema Msigwa na kuongeza:
 
“Tulitarajia Waziri Mkuu awe wa kwanza kutafakari na kujipima kama kweli anastahili kubaki hasa baada ya madudu yale ambayo yameichafua Serikali mbele ya umma.”
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alisema wakati umefika kwa Waziri Mkuu, Pinda kukaa pembeni na kumwachia Rais Kikwete aunde safu nyingine.
 
“Pinda ni mtu wangu. Tunaheshimiana na sina chuki naye. Kwanza yeye ni mmoja wa watu ninaotuhumiwa kuwapa jimbo apite bila kupingwa na kuniletea matatizo kwenye chama changu.
 
“Hivyo sina chuki naye maana pia anatoka kanda yetu. Hata hivyo, hali ya sasa ya nchi inahitaji kupumua. Ampe nafasi Rais aunde Serikali upya.”

Alisema kuna tatizo kubwa la uongozi ndani ya nchi na kuwa mambo hayaendi licha ya juhudi mbalimbali pamoja na Bajeti ya Serikali kuongezeka kila kukicha.
 
“Huduma hazifiki kwa wananchi. Serikali ni kama haipo, nchi imevimba na inahitaji kupumua. Mwaka 1990 Rais Mwinyi (Ali Hassan Mwinyi,) alikumbwa na hali kama hii na Warioba alijiuzulu ili kumpa nafasi kuunda upya Serikali. Alimrudisha Warioba lakini mawaziri wengi waliondoka,” alisema Zitto.
 
Aprili mwaka jana katika mazingira yanayofanana na ya mkutano wa 14 wa Bunge uliomalizika Jumamosi, wabunge 74 wakiwamo wa CCM walitia saini fomu ya kutaka kumng’oa Pinda.
 
Hata hivyo, aliepuka zahama hiyo, baada ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri mwezi mmoja baadaye na kuwaondoa mawaziri sita na manaibu waziri wawili waliokuwa wakishinikizwa kuachia ngazi.
 
Mawaziri hao walikuwa William Ngeleja (Nishati na Madini), Mustafa Mkulo (Fedha), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), Omar Nungu (Mawasiliano), Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara) Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii).

  Manaibu walikuwa Dk Athuman Mfutakamba (Uchukuzi) na Dk Lucy Nkya (Afya na Ustawi wa Jamii).

>>Mwananchi

HII NDO KAULI YA MANJI BAADA YA KIPIGO CHA JANA TOKA KWA SIMBA CHA BAO 3-1


Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji ameaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa
Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji. 
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anaapa hongera kwa kushinda bonanza la jana, anasema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi  majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.

KIJANA ANUSURIKA KUUWAWA MARA DAADA YA KUTAKA KUIBA PIKIPIKI...!! TAZAMA MAPICHA HAPA..

 Mtu aliyetuhumiwa kujaribu kuiba pikipiki aina ya Bajaj maeneo ya Coco Beach Dar es Salaam akiwa tahabani baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi maeneo ya 
Msasani jirani na Hospitali ya CCBRT hivi karibuni. Kwamujibu wa mashuhuda wa tukio hilo kijana huyo alikubwa na mkasa huo alipokuwa katika harakati za kukimbia na inadaiwa alikuwa na hirizi inayomsaidia kuendelea kupumua. Askari wa Kituo cha polisi cha Oysterbay walifanikiwa kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala na tutawajuza kama anaendelea na hali gani. Kwa mujibu wa askari wa Kituo hicho wamethibitisha kumfikisha hospitalini na kwa kuwa hakuna anayemtuhumu baada ya kupata kipigo kikali watafanya mchakato wa kumlinda mpaka atoke hospitalini.

JAMAA AKAMATWA KWA KUOA MTU NA MDOGO WAKE ALAFU WOTE NI WANAFUNZI...!!

Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba (kushoto) akipitia kitabu cha orodha ya matukio ya dawati hilo. Kulia ni msaidizi wake.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba (kushoto) akipitia kitabu cha orodha ya matukio ya dawati hilo. Kulia ni msaidizi wake.
Na Joachim Mushi, Nkasi JESHI la Polisi Wilaya ya Nkasi kupitia dawati la Jinsia na Watoto, linamshikilia Pius Jacob Mkazi wa Kijiji cha Chala kwa kosa la kuoa mtu na dada yake, ambapo mdogo mtu alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kabwe wilayani Nkasi. Jacob alikamatwa na Polisi wa Dawati la Jinsia na watoto Kituo cha Nkasi ikiwa ni wiki moja tangu amchukue kwa nguvu binti huyo wa darasa la tano (umri miaka 12) na kuja kuishi naye kama mke na mume huku akiwa tayari amemuoa binti mwingine wa kwanza mwenye umri wa miaka 16 ambaye pia ni dada wa binti wa pili. Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Dawati la Jinsia Nkasi, CPL-Anna Kisimba alisema walimfuatilia Jacob na kumkamata baada ya wao kupewa taarifa na mmoja wa majirani wa mtuhumiwa kuwa alikuwa akiishi kinyumba na wanafunzi hao. “…Tulikuwa katika ziara zetu za kawaida zilizoambatana na siku 16 za kupinga ukatili tukizunguka baadhi ya vijiji vya wilaya yetu, ndipo raia wema walituarifu kuwepo kwa tukio hilo na kuanza kufuatilia hatimaye kumkamata mtuhumiwa,” alisema Kisimba.
Tayari mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desenba 10, 2013 kwa kosa la kumuoa mwanafunzi na kubaka katika Mahakama ya Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa kujibu mashtaka ya tuhuma zake.
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Nkasi, Oscar Mdenye alisema baada ya kufuatilia zaidi wamebaini hata binti (16) aliyemuoa wa kwanza alikuwa ni mwanafunzi haijulikani alitumia mbinu gani za kumpata na kuanza kuishi naye kama mke na mume. Aidha ameongeza kuwa kwa mujibu wa tarifa ambazo walizipata kutoka kwa majirani inadaiwa binti wa pili alimpata kwa kutumia nguvu na vitisho, kwani alimfuata nyumbani kwao na kudai anakuja kuwasalimia lakini baada ya kufika kwake alimjulisha binti huyo kuanzia sasa wewe ni mke wangu na kuanza kuishi naye. “…Hadi Polisi na Ofisi ya Ustawi wa Jamii tunafikiwa na taarifa hizo inadaiwa mtuhumiwa huyu alikuwa tayari ameishi na binti huyu wa pili kwa wiki nzima nyumbani kwake, na majirani walijua baada ya binti wa pili (12) kuanza kulalamika kwao kuwa alikuwa amechukuliwa kwa nguvu na kulazimishwa kuolewa,” alisema Mdenye. Juhudi za kumpata mtuhumiwa kuzungumzia tuhuma zake hazikuweza kuzaa matunda baada ya kuwa mahabusu akisubiri mwenendo wa kesi yake inayomkabili. Hata hivyo matukio ya ukatili yanayoripotiwa polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Nkasi yamekuwa yakipungua kutoka mwaka hadi mwaka, kwani kwa mujibu wa takwimu za dawati hilo kwa mwaka 2012 kulikuwa na kesi 224 za ukatili zilizoripotiwa, ilhali kwa mwaka 2013 jumla ya kesi 143 zimeripotiwa wilayani hapo.
Source: The habar

 
Design by Jambo Tz