Showing posts with label mapenzi. Show all posts
Showing posts with label mapenzi. Show all posts

MKE WANGU AME-LOCK SIMU YAKE KWA PASSWORD..NAHISI KUIBIWA

''Nampenda sana mke wangu, ni miezi sita tu toka tufunge ndoa!!!

sitaki kumuudhi wala kumkera kwa lolote, namtimizia kila kitu ili mradi tu asipate vishawishi vya kutoka nje ya ndoa!

toka tuanze mahusiano yetu ya kindoa, mke wangu alikuwa msikivu sana kwangu, kila ninalo mwambia amekuwa 

akinisikiliza! ilifikia kipindi ikawa ni utamaduni wetu kuwa tuna share mpaka simu zetu! yeye akiwa anatumia yangu mi 

natumia yake! wiki chache hivi zilizopita, nimeshangazwa sana na hiki kitendo nilichokuta kwenye simu ya mke wangu, simu yake imefungwa kwa namba maalum anazozijua yeye mwenyewe!! nilipojaribu kuhoji juu ya hilo, akanijibu kwa ukali, ''kwani wewe unataka nini, simu si yangu, na wewe una yako.. funga na wewe yako''!

niliamua kukaa kimya ili nisizue mengine! mke wangu amekuwa ni mtu wa kupokea simu za ajabu ajabu na kutumiwa meseji kila mara, kila ninapohoji, yeye anasema kwa ukali kwamba wivu, namwaibisha kwa mashoga zake... eti tuko mjini hapa!!!

mwenzenu nimechanganyikiwa!!! nahisi kunyang'anywa tunda langu''....

BINTI ALIYE DAIWA KUVUNJA NDOA YA BOB JUNIOR AKANUSHA NA KUSEMA HAYA...

 

Baada ya Blogs na Magazeti Kumwandika sana Ashley Toto  Mwanadada Kutoka Kenya Kuhusika na Kuvunjika kwa ndoa ya Bob Junior Amejitokeza na Kuandika haya kwenye Wall yake ya Facebook
"****JAMANI NIMECHOKA NA SKEDOLS ZA UONGO ILA NAAMINI HII NI MITIHANI NA INSHAALLAH YATAISHA***I HAVE NOTHING TO DO WITH HIM...." 

Tuliamua kumtafuta na kuongea nae na kusema kwa masikitiko kuwa Hana uhusiano wa kimapenzi na Bob Junior Bali wao ni marafiki tu wa Muda mrefu..Pia akasema huwa anamtafutia Show Sehemu mbali mbali ikiwemo Ujerumani anapoishi ..... So anasema amechoka kuandikwa kuhusu Bob Junior


JE, NI KWELI KUWA KILA MWANAMKE ANAJIUZA NA SIO WALE TU WANAOSIMAMA BUGURUNI??

 
Huu ni ukweli hata tukipinga hakuna mwanamke asiyejiuza tofauti kuna aina mbili tu za hii biashara.
1. Wale wanaojiuza kwa kutafuta wateja kusimama mabarabarani. 2. Hawasimami barabarani wanaenda kwa special order, kufahamiana kwanza kama urafiki, kupitia mitandao, kukutana kwenye bar na magari n.k
Ukitaka kujua kuwa wote hawa wanajiuza, mlale mwanamke halafu usimpe noti uone zali litakavyokuwa! Fanya uchunguzi hapahapa jijini Dar, nakuhakikishia ni wanawake wachache sana labda 2%-10% ambao hawako kibiashara juu ya mapenzi.
1. Kuna demu mzuri sana anafanyakazi (ofisi kubwa) ya sirikali mshahara wake ni zaidi ya Tshs m2 kwa mwezi anabwana ake tena wameshibana lakini juzi tu akawa anataniwa na rafiki yangu mmoja mwenye nchi ndafuu sana kuwa nataka kukuoa, kama vipi uje home tuonje tunda bana, tena demu aliweka mafuta yake akaja na gari yake akavurugwa kisa uanjua nini hapa?? Pesa huyu anajiuza ila yeye ni kwa investiment huyu ni MUWEKEZAJI!!
2. Kuna demu anasoma chuo kikuu anatamba sana kwenye mitandao na kuweka picha ya bwana ake kila mara juzi kati mchizi wangu kamuanzishia chat kwa fb mpaka muda huu kashatoa uroda biashara ni ileile kila akitaka kutoa nauli, alipewa mara ya kwanza elfu 20 alikasirika sana, huyu ni mjasiriamali.
3. Nenda Bar yoyote Dar, hata mhudumu unayemuona anajiheshimu akikuletea soda au bia yako mnong'oneze mwambie nina lfu 50 tukalale wote, hakikisha una simu maana tayari mzigo umepata hii nayo ni biashara anauza sema tu ni parti time.
4. Usimuone mmama wa makamo mkubwa na mkurugenzi wa kampuni fulani mwambie ninajua kula mzigo lazima utampata tu wewe usiogope sura yake na heshima yake ongea tu, huyu naye anauza sema yeye ni doner.
5. Mademu karibia 80% Dar wanamabwana zaidi ya 5 kila mmoja amepengwa kisawasawa, kweli anao watano aende buguruni kufanya nini? 

Hata mkikataa mnajiuza tena mnajiuza vibaya sana dunia imeisha tu

JE, PENZI LAKO LIMECHUJA, UNAJUA CHANZO...?? SOMA HAPA..



Leo nitazungumzia suala la penzi kuchuja. Ipo hali ya kujisahau baada ya wapenzi kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, haieleweki kama ni tabia ya mtu ama ni uhalisia wa mambo kwasababu ukweli ulio wazi ni kwamba, mwanzo wa uhusiano wengi hujitahidi kufanya mambo mengi ya kuwafurahisha wapenzi wetu lakini kadiri siku zinavyosogea, penzi huanza kuchuja.
Kama huamini katika hili, rudisha nyuma kumbukumbu zako kipindi kile ambacho ndio jamaa kaamua kukueleza wazi kwamba anakupenda halafu angalia na sasa hivi, utabaini kwamba kuna tofauti kubwa sana.
Huenda mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi, chokoleti tabia hiyo huenda ikawa imeyeyuka, hakuna kati yenu atakayekumbuka kitu hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati ndiyo huendelea kuzingatia hayo.
Kuna wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi ambapo kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie jinsi  alivyo fundi wa 'kuyarudi' ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manjonjo huadimika kabisa.
Kawaida yenu ilikuwa kubadilisha hoteli kwa ajili ya chakula cha jioni lakini tabia hiyo hutoweka, labda kila wiki ilikuwa lazima muende 'out' mara tatu katika kumbi tofauti za starehe na kufurahia mapenzi yenu, hali hiyo itabaki historia tu.
Hivi hujawahi kusikia mtu anasema "Enzi zile naanza uhusiano na mpenzi wangu mapenzi yalikuwa moto moto, kila wiki ilikuwa lazima twende beach lakini, siku hizi nikigusia tu kwenda huko ni ugomvi."
Maneno kama haya huwa yananiuma sana hasa ninapogundua kwamba walio wengi wanakuwa na nguvu ya soda pale wanapoingia katika uhusiano lakini baada ya muda mambo hubadilika kabisa.
Sijajua ni kwasababu gani lakini kwa utafiti mdogo ambao nilioufanya kwa baadhi ya wanaume ni kwamba, wao wanapofanikiwa ‘kuona ndani tu’ hujenga kiburi fulani kwa wasichana wao huku wakiamini kwamba, hata wawe tofauti vipi hawawezi kuachwa!
Labda nijaribu kushauri kitu katika hili kwamba, kama uko kwenye uhusiano wa kimapenzi ama uko ndani ya ndoa, unatakiwa kufanya kila linalowezekana kulifanya penzi lenu lisichuje.
Wewe ndio unaweza kulifanya likaendelea kuonekana kuwa jipya kila siku ama kulifanya likachuja mithili ya nguo inayochuja rangi iliyotumbukiza katika ndoo ya maji ya moto.
Hatukatai kwamba, kuna mabadiliko ya kimaslahi, pengine mtu na mpenzi wake wameketi na kuona wanatumia pesa nyingi viwanja, kwahiyo wanaamua kupunguza au kuacha ili kujenga maisha bora ya baadae, si unajua tena mnapokuwa na malengo ya kimaisha zaidi?
Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, penzi la dhati haliwezi kuchuja hata siku moja. Tujue wapo ambao wameishi miaka zaidi ya hamsini lakini penzi lao bado ni moto licha ya kuwepo kwa mabadiliko madogo ambayo hayakwepeki kutokana na umri.
Yapo mabadiliko mengi, lakini zaidi tujirekebishe, tukumbuke kwamba baadhi ya vitu tulivyokuwa navyo huko nyuma ndivyo viliwavutia wepenzi wetu na kukubali kuwa nasi kwa hiyo tukiacha tunakuwa tunawakatili.

JE UNATAMANI KUMUACHA MPENZI WAKO, KWA SABABU MOJA AU NYINGINE...?? CHUKUA MUONGOZO HUU..


Upo uhusiano ambao umelengwa kudumu, hasa kwa wanandoa. Kuna wengine hawa sura ya kudumu, wapo kwa muda kwa kuzingatia mazingira pamoja na kile kilichomo ndani ya nafsi zao.

Unaweza kujiuliza; Kwanini ufike wakati utake kuvunja uhusiano wako na mwenzako? Iwe kirafiki au kimapenzi, Ipo wazi kwamba kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuwafanya wahusika kuamua.

Yawezekana uhusiano wako na mpenzi wako au rafiki yako wa jinsia tofauti unakutia hasara, au unakuharibia biashara, au unakupunguzia heshima katika jamii, au pengine uaminifu wako kazini. Mathalan, mpenzi wako anapokuwa anafahamika kuwa ni kahaba.

Inawezekana uhusiano wako na mwenzako unaidhuru nafsi yako. Mfano, mwenzio ana nguvu sana juu yako kiasi kwamba huwezi kusema “hapana” kwa lolote analokwambia. Pengine kutokana na hali hiyo umekuwa ukilazimika kufanya mambo ambayo huyapendi na ambayo hayaendani na maadili.

Lakini pia yawezekana umeanza kumchukia mwenzako. Mazingira yamebadilika, kwahiyo wewe na yeye hampatani tena. Unajitazama na kugundua kwamba ulivyo huendani naye. Ni matokeo ya kuchokana!

Naam, baadhi ya mahusiano, yawe ya kirafiki au kimapenzi, huwaweka katika wakati mgumu watu kiasi kwamba ni lazima mtu achukue hatua ili aweze kuishi kwa amani na furaha ya kweli. Hata hivyo, ikae akilini kwamba inauma mno kuachana na mtu unayempenda!

Kumaliza uhusiano wa kimapenzi au kirafiki si hatari, lakini la msingi ni kuhakikisha kuwa unamwacha mwenzako akiwa hajaathirika kisaikolojia kwa namna yoyote. Kwa sababu hiyo unapaswa kujifunza njia sahihi ya kumaliza uhusiano wako na mwenzako inapobidi.

Kuna jamii inaweza kuthubutu kusema, unapochoshwa na mtu, mchukue uende naye mahali kisha umueleze kwa uwazi kuwa hutaki tena kujihusisha naye kwa sababu moja, mbili, tatu. Hata hivyo, hilo si jambo rahisi kwa wengi.

Badala ya kukubaliana na mtu ana kwa ana na kumweleza kuwa humhitaji tena, zipo njia za kirafiki na za kidiplomasia ambazo unaweza kuzitumia na kumaliza mambo bila kusababisha matatizo makubwa au madhara yoyote ya kisaikolojia.

WEKA SABABU ZAKO MEZANI!
Unapotaka kumbwaga rafiki yako au mpenzi wako ambaye hujampa ahadi yoyote ya kuishi naye katika ndoa, anza mchakato kwa kuweka bayana sababu zinazokufanya utake kuachana naye. Hakikisha kuwa sababu unazoziweka ni zile ambazo mpenzi wako huyo hatapata namna ya kuzipinga.

Zitengeneze sababu hizo kwa kuzingatia mtazamo wako mwenyewe, na si kwa mtazamo wa mpenzi au rafiki yako huyo, ili hatimaye kusiwe na sababu ya mwenzako huyo kudhani atajirekebisha ili aweze kuendelea kuwa na wewe.

Namna hii utakuwa unayaangalia zaidi maslahi yako mwenyewe na iwapo utalazimika kumweleza mwenzako ni kwa nini unataka kumaliza uhusiano wako na yeye, sababu zako hazitaonekana kama shambulio kwake yeye mwenyewe wala tabia yake.

USITHUBUTU KUWASILIANA NAYE!
Utakapaokuwa umeweka wazi sababu zako na kuziamini, weka mkakati kuwa hutaanzisha tena mawasiliano na mwenzako. Jiwekee msimamo kuwa hutampigia simu, wala kumtumia ujumbe wa simu, wala baruapepe na kadhalika, ila utajibu tu yeye atakapoanzisha.

Unapomwalika mtu au kumpigia simu au kumtumia ujumbe ni kama unamtia moyo na kumfanya aamini kuwa unampenda na kumjali. Kama mhusika ni mtu mwenye fahamu atashtuka kuwa jitihada zote anafanya yeye na wewe uko kimya. Akitafakari atagundua kuwa hauko naye tena.

AKIKWITA KATAA!
Iwapo kweli umedhamiria kumaliza uhusiano wako na mwenzako, jaribu kukataa mialiko anayokupa, mathalani kwa ajili ya chakula cha pamoja cha mchana. Pia kama atasema atakufanyia jambo Fulani, kataa kiaina.

Fanya vivyo hivyo kwa matukio yote ya kijamii. Kataaa mialiko kwa njia ambayo hatkushtukia haraka kuwa humhitaji tena, bali aje kushtuka baadaye atakapojumlisha matukio.

Katika hatua za awali, hii itamaanisha kuwa utakosa kwenye matukio Fulani ambayo wewe mwenyewe ungependelea kuyahudhuria, lakini huna la kufanya, maana umeazimia kumaliza uhusiano wako na mpenzi au rafiki yako.

Unapotaka kupeleka ujumbe kwa mpenzi wako kuwa hayuko tena moyoni mwako, lazima tu ujitoleee kupata hasara katika baadhi ya mambo. Kumbuka kuwa huhitaji tena uhusiano wako na mwenzako.

 
Design by Jambo Tz