INASIKITISHA, MWANAMKE ATOLEWA MAWE SITA TUMBONI, TAZAMA HAPA!!

Mwanamke mmoja nchini Czech Republic ametolewa mawe takribani sita katika tumbo lake baada ya kufanyiwa oparesheni kubwa ya upasuaji na madaktari bingwa.


Madaktari wanasema alikuwa na hofu kubwa ya kuona madaktari kwa sababu ni nusu kifo ilikuwa ni kufa au kupona.
Alikaa na tumbo hilo kwa miaka 47 na lilikuwa likizidi kuvimba siku hadi siku ni mara 20 la tumbo la kawaida.
Wataalamu wanasema kwamba haijulikani kama atapata nafuu ya haraka na moja kwa moja ila baada ya oparesheni uzito wake ulipungua kwa kasi.
Mwanamke huyo raia wa Czesh alikuwa na takribani mawe sita ambayo yalioonekana na kutolewa kutoka kwenye tumbo lake na ukubwa wa tumbo ulikuwa mara ishirini la tumbo la kawaida.

Mwanamke huyo alifanyiwa oparesheni ya kuokoa maisha yake katika hospitali ya mkoa wa Zlin mwezi uliopita.
Ilichukua upasuaji wa zaidi ya saa saba kuondoa ukuaji ambao ni zaidi ya mita moja katika mduara wa kipimo cha kawaida.
Zdenek Adamik , mkuu wa Idara ya masuala ya uzazi na magonjwa ya wanawake katika hospitali hiyo, alisema madaktari walikuwa walishangazwa kwa nini mwanamke huyo akutafuta msaada wa matibabu mapema.“Ni ajabu kwamba familia na marafiki wa karibu hawakuweza kupeleka taarifa katika mamlaka za utabibu mapema au kuguswa na matatizo ya mama huyo,” alisema mkuu huyo wa idara.

Chupa za Damu zilizotumika kumwogezea Damu mama huyo wakati wa Oparesheni iliyodumu masaa saba.

UMEWAHI KUJIULIZA KWANINI NYIMBO AU VIDEO ZA "DIAMOND" AZIPIGWI "CHANNEL TEN" AU "MAGIC FM" KWA MWAKA SASA..SOMA SABABU HIZO HAPA

Diamond akiwa katika studio za Magic FM
Kama umewahi kujiuliza kwanini ulikuwa husikii nyimbo za Diamond Platnumz kupitia kituo cha Magic FM cha Dar es salaam pamoja na kituo cha TV Channel Ten kwa kipindi kirefu, jibu ni kwamba msanii huyo ambaye nyota yake inazidi kung’ara kila kukicha aliwahi kukikosea kituo hicho, kwa lugha ya mtaani ‘alizingua’.
Kwa mujibu wa Salmamsangi.com, Jumatano ya wiki hii (Jan 8) kupitia kipindi cha Daladala Beats cha Magic FM, Diamond akiwa Live kwenye kipindi hicho aliomba msamaha na kusema kuwa alikuwa na tofauti na Radio hiyo kutokana na mambo ya kibinadamu.

Diamond ambaye wiki hii ameachia video na audio ya ‘Number 1 RMX’ aliyomshirikisha Davido wa Naija, alifika katika studio za Magic akiwa ameongozana na Meneja wake Babu Tale wa Tip Top Connection pamoja na Said Fella.

Baada ya kuomba msamaha hewani sasa nyimbo za Platnumz zimeanza kupata airtime kupitia vipindi mbalimbali vya Radio hiyo ambayo ilisitisha kupiga kazi zake kwa takribani mwaka mmoja na nusu toka tofauti hizo zilipojitokeza

HUYU NDIYE MTANGAZAJI ANAMILIKI JUMBA KALI ZAIDI LA HUKO MAREKANI, TAZAMA PICHAEllen DeGeneres ndio wanasema mtangazaji anayeishi kwenye jumba kali zaidi huko L.A Marekani. TMZ wame ripoti kuwa jumba hili ni kali na lenye thamani kubwa zaidi kuliko jumba lake la awali alilonunua. 


Jumba lake la sasa lina thamani ya dola milioni $39,888,000 na linaitwa The Brody House. Kiwanja kina eka 2.3 , vyumba sita vya kulala, mabafu sita, bwawa la kuogelea , sehemu ya mazoezi na uwanja wa kucheza tennis.

WAZIRI PROF. MAGHEMBE AJIUZULU; DAWASA/DAWASCO WAREJESHA HUDUMA NDANI YA WIKI MOJA KATIKA MAENEO YALIYOKUWA YAKIPATA MGAWO WA MAJI KABLA

CHADEMADirectorofInformationandUbungolegislatorJohnMnyika1
Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA) Mh. John Mnyika.
Nimemtumia ujumbe Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe kumshauri ajiuzulu kutokana na kujirudia rudia kwa matatizo ya maji katika Jiji la Dar Es Salaam kinyume na maelezo yake ya uongo  aliyoyatoa bungeni tarehe 4 Februari 2013.
Aidha, Wenyeviti wa Bodi na Watendaji wakuu wa Mamlaka zinazohusika na huduma ya maji jijini (DAWASA na DAWASCO) watoe maelezo kwa umma juu ya sababu za kweli za matatizo ya maji kujirudia rudia katika Jiji la Dar Es Salaam.
Pia, wajieleze kwa umma ni kwanini wananchi wasipendekeze Rais awachukulie kwa uzembe, kuisababishia hasara Serikali, kuathiri  uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa kukosa maji mara kwa mara ambayo ni huduma ya msingi ya binadamu na malighafi muhimu katika uzalishaji.
Itakumbukwa kwamba tarehe 4 Februari 2013 niliwasilisha hoja binafsi bungeni juu ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji katika jiji la Dar Es Salaam, nikipendekeza Bunge kuingilia kati kuweza kuisimamia Serikali kuchukua hatua za haraka.
Iwapo hoja hiyo ingejadiliwa na maazimio yote kutekelezwa matatizo ya maji katika Jiji la Dar Es Salaam mpaka hatua ya sasa yangekuwa yamepungua katika maeneo mbalimbali kutokana na hatua ambazo nilipendekeza zichukuliwe.
Hata hivyo, badala ya kuunga mkono hoja hiyo ambayo ingeisaidia Wizara yake  na kurekebisha udhaifu uliokuwepo na hivyo kumrejeshea imani kwa umma ambavyo ilikuwa imepungua; Waziri Maghembe akaamua kinyume cha kanuni za Bunge kutoa hoja ya kuondoa hoja niliyowasilisha.
Katika hatua hiyo nilijaribu kutumia kanuni za Bunge kuweza kutoa ufafanuzi juu ya uongo wa Waziri Prof. Maghembe na hatua ambazo Bunge lilipaswa kuchukua. Hata hivyo Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai aliamua kukiuka kanuni kumlinda hali ambayo ilichochea vurugu bungeni.
Mara baada ya kurejea bungeni tarehe 10 Februari 2013 nilihutubia wananchi na kuwaeleza kusudio la kuandaa maaandamano kwenda Wizara ya Maji iwapo katika kipindi cha ndani ya wiki mbili Waziri Prof. Maghembe asingejitokeza kutoa maelezo kwa umma kuhusu masuala yote ambayo alipaswa kuyajibu bungeni juu ya hatua za haraka zilizopaswa kuchukuliwa.
Ndani ya wiki hizo mbili Waziri Maghembe alijitokeza mara mbili kuzungumzia masuala ya maji Dar Es Salaam; kupitia mikutano ya CCM ikiwemo katika kata ya Goba jimboni Ubungo na katika mkutano wake na wafanyakazi DAWASA na DAWASCO tarehe 21 Februari 2013 na kueleza hatua za haraka ambazo angesimamia zichukuliwe.
Hata hivyo, baada ya wiki moja bila ya Waziri wa Maji na Wizara kwa ujumla kuonyesha  kwa matendo kuisimamia kwa karibu EWURA, DAWASA, DAWASCO na Manispaa ya Kinondoni kuchukua hatua za haraka ambazo nilizieleza kwenye hoja binafsi, niliamua kuchukua hatua zaidi.
Nilitangaza kuongoza maandamano ya wananchi tarehe 16 Machi 2013 kwenda Wizara ya Maji ili kupata majibu na kuisimamia Serikali kuchukua hatua za haraka. Hata hivyo maandamano hayo yalizuiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu zisizo za msingi na kuombwa kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Nilikata rufaa lakini toka wakati huo mpaka anaondelewa katika nafasi yake Waziri Dr Emmanuel Nchimbi alikwepa kuchukua hatua dhidi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela kwa kuvunja sheria, kusababisha hasara na kuwanyima haki ya msingi wananchi ya kufikisha ujumbe kwa Serikali.
Maandamano hayo yangefanyika na hatua kuchukuliwa matatizo yangepungua tofauti na ilivyo sasa, hivyo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima anapaswa kueleza umma lini rufaa hiyo itashughulikiwa maandamano yaweze kufanyika wananchi wapate majibu ya hatua za haraka nilizopendekeza ndani na nje ya Bunge.
Zaidi ya nusu mwaka umepita toka Waziri Prof. Maghembe atoe ahadi ambazo ameshindwa kusimamia utekelezaji wake na hivyo kupaswa kujiuzulu. Iwapo Waziri Prof. Maghembe hatajiuzulu nitaeleza hatua zaidi ambazo nitachukua.
Wakati hatua hizo zikisubiriwa, natoa mwito kwa DAWASA na DAWASCO kuhakikisha kwamba katika kipindi kisichozidi wiki moja huduma za maji zinarejea katika maeneo ambayo yalikuwa yakipata mgawo wa maji.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
10/01/2013

RC Manyara ajikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa

 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo, amejikuta katika wakati mgumu baada ya wananchi wa wilaya ya Kiteto,  kumzomea na kumtaka aondoke na mkurugenzi wake wakati alipokutana nao kuzungumzia  mgogoro wa wakulima na wafugaji.

Hali hiyo ilijitokeza wakati mkulima,  Ramadhani Machaku, aliposimama kuuliza swali, lakini Mkurugenzi wa Wilaya ya Kiteto, Jane Mutagurwa, kumnyang’anya kipaza sauti na kumtaka aulize swali badala ya kutoa hotuba.


Katika swali lake Machaku, alishutumu uongozi wa wilaya kuwa umechangisha mamilioni ya fedha kwa wafugaji ili kuhakikisha wakulima wanaondoka na matokeo yake kule mashambani wanaishi kama maadui na kuuana kinyama.


Aidha alisema kuwa viongozi wamekuwa hawataki kuongea ukweli kuhusu jambo hilo na kudai kuwa hawataondoka katika eneo hilo hadi hapo serikali itakapowahakiki wafugaji ambao ndiyo waliowauzia maeneo.


Alimuomba Rais Jakaya Kikwete au Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati kutatua mgogoro huo kutokana na viongozi wa wilaya hiyo kuwagawa wananchi na kupindisha ukweli.


Hatua ya mkurugenzi huyo kumnyang’anya kipaza sauti, kiliwakasirisha wananchi hao, ambao walianza kuzomea  huku baadhi wakisusia na kuanza kuondoka  kwenye mkutano huo, wakitaka Mkuu wa mkoa aondoke na mkurugenzi wake.


Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kiteto, Foka Dinya, aliingilia kati na kuwataka wananchi hao kuacha vurugu.


 Awali  Mbwilo ambaye alitoa fursa kwa wananchi kuuliza maswali, alikiri kuwa mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Kiteto unasababishwa na viongozi wa wilaya hiyo na kuiagiza kamati ya ulinzi ya mkoa kukaa kuangalia tatizo ili wilaya hiyo iwe na amani.


“Mambo haya tangu mwanzo nayafahamu lakini bado tunayafanyia kazi lakini ni kwa nini watu wanakubali kuchangishwa fedha bila ya utaratibu wa serikali na bila kibali maalum sisi kama serikali tunalifuatilia haiwezekani michango ichangishwe kikabila,”alisema.


Alisema kuwa  serikali ya mkoa inatambua suala hilo la viongozi kuhusika na mgogoro huo.


Alisema kuwa tangu juzi amefanya ziara na kupokea malalamiko na taarifa kuwa viongozi wa wilaya walipokea rushwa ya madume ya ng’ombe kutoka kwa wafugaji ili wakulima waondolewe katika Hifadhi hiyo.


“Wananchi kweli mmegawanywa katika makundi na inawezekana ni sisi viongozi ndiyo tuliofanya hivi na matokeo yake wafugaji wanaona wana haki ya kukaa ndani ya hifadhi huku wakulima nao wanaona wamehujumiwa kwanini wafugaji wakubaliwe,” alisema Mbwilo.


Alisema kuwa mgogoro huo ulitokana na baadhi ya wakulima kuingia katika eneo la hifadhi kinyume na sheria na kujichukulia ardhi kubwa mpaka kumiliki hekari 6000.


Aliwataka wakulima na wafugaji kuondoka katika hifadhi hiyo mpaka hapo watakapofanya utaratibu wa kugawa tena kulingana na vielelezo  watakavyowasilisha kuwa walipewa idhini na nani ya kumiliki maeneo hayo.


Aliwaagiza viongozi wa wilaya kuwaondoa katika eneo hilo wakulima na wafugaji wote kwa pamoja kwa kuwa wameingia kinyume na sheria tofauti na agizo la awali ambalo liliwataka wakulima kuondoka.


Awali mmoja wa wafugaji wa jamii ya Kimasai, Kisioki Masiyai, alisema kuwa chanzo cha mgogoro na kusababisha mapigano ni Mkurugenzi wa wilaya hiyo, ambaye aliwachangisha fedha wafugaji ili kuwaondoa wakulima.Alisema kuwa hawatakubali kuondoka katika hifadhi hiyo mpaka hapo serikali ya wilaya hiyo itakapotoa mchanganuo wa matumizi ya mamilioni ya fedha ambazo walichangishwa wafugaji.
 

CHANZO: NIPASHE

'Afufuka baada ya kujitoa uhai' AJIKUTA AKIWA KWENYE CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI


Mgonjwa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Naivasha

Wananchi wa Kenya wameshangazwa na taarifa ya mwanamume mmoja aliyedhaniwa kuwa mfu kufufuka kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu Nairobi.

Mwanamume huyo Paul Mburu mwenye umri wa miaka 24, alipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai,kutokana na ugomvi wa kinyumbani na babake ingawa alisemekana kufariki Jumatano usiku wakati akipokea matibabu.
Wafanyakazi wa hospitali hiyo walipigwa na butwaa na hata kutoroka walipoona mwili wa mtu aliyedhaniwa kufariki ukisonga na kuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Afisaa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo ya wilaya, Dokta Joseph Mburu, alisema kuwa dawa iliyotumiwa kumtibu Mburu hufanya moyo kupiga polepole hali ambayo huenda ilimfanya muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.
Mwanamume huyo alisikika akimtaka mmoja wa wafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na hapo ndipo mmoja wa wafanyakazi alipotimua mbio kwa hofu.
Nusura Mburu awekwe kwenye jokovu la kuhifadhia maiti.
Jamaa za mwanamume huyo akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha maiti siku ya Alhamisi ili kujiandaa kwa mazishi , lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa hai.

HIVI NDIVYO WEZI WALIVYOLIFANYA GARI LA DJ FETTY ASUBUHI YA LEO

Janga la kwanza 2014, nje ya home saa 12 asubuhi, makaka wezi wanne na gari lao wamekuja, wamevunja kioo na wakaanza kufungua side mirror, bahati mjumbe katoka, akawauliza nyie vipiii, ndo wakatoka nduki wakaingia kwenye gari lao

walililokuwa wamelipaki karibu na gari langu nankuseoa kwa speed 120, hawajafanikiwa kuondoka na chochote...hawakukamatwa ila wangekamaaaaatwa.....hahahahahaa, hivi ndo nimeianza asubuhi ya leo. Shout out kwa mjumbe wangu bila ya yeye duuuh nahisi ningelikuta gofu!!!

NAOMI CAMPLE ATUAKENYA KWA AJILI HII...SOMA HAPA

Super model  Naomi Campell ameonekana  huko Pwani ya kenya. Kwasasa Kenya inahali nzuri ya hewa na macelebs wengi hupenda kuja majira haya kwa ajili ya mapumziko.Model Huyu mwenye umri wa miaka 43 si kwamba yupo kwa ajili ya mapumziko tu bali ameamua kujumlisha mapumziko yake na shughuli zake zakihumanitarian kusaidia watoto yatima nchini kenya.
naomi campell
naomi-malindi
Naomi alikua Nchini Kenya tokea mwishoni mwa mwaka 2013 na aliweza kukutana na watu wengine maarufu huko pwani ya malindi kama Flavio Briatore,63  ambaye ni mfanyabiashara maarufu nchini italia ambaye naye alikua mapumzikoni kwenye pwani hizo za malindi.
Naomi-Flavio-Briatore

PICHA ZA FAMILIA YA JAJI LAN MBUGUA WA TUSKER PROJECT FAME...ANGALIA PICHA HAPA

553698_10151049689310266_1105956410_n
Judge Ian Mbugua has always been known to be a no nonsense man especially in the last six episode of Tusker Project Fame that he has served as a Judge. Many love him, many fear him and many also
hate him but he does not seam to care much, as long as he expresses his opinion and does his work as is expected of him, people will talk and talk but he will remain to be who is.
ian2
Apart from the other things that this no nonsense Judge is known for, he has another side of his life. He is a family man. A loving father to three very beautiful, youthful kids and a loving husband to one wife. Below are some amazing pictures of this amazing family.
ian4 ian3 ian1
Source: http://niaje.com

TAZAMA PICHA ZA MISS BOOTY 'VERA SIDIKA' WA KENYA KABLA NA BAADA HAJAWA MISS BOOTYEver wondered how your favorite celebrity looked like way back before they could afford designer clothes, the best kind of makeup and hair. Were they geeky? Were
they weird looking or were they still as stunning? I came across a picture of Vera Sidika before all the fame and glamour and like most of us; she really started from the bottom

Started from the bottom....................................Now we are here!
CREDIT-Ghafla.co.ke

MCHEZAJI WA BAYERN MUNICH NA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI AJITANGAZA KUWA SHOGA

thomas 1Nyota wa zamani wa Ujerumani Thomas Hitzlsperger aliyeanzia soka lake kwenye klabu ya Bayern Munich  amejitangaza kuwa shoga.
Aliwahi kucheza kwenye ligi ya England kwa muda wa miaka mitano akicheza kwenye klabu ya Aston Villa kabla ya kujiunga na VFL Stutgart ya nyumbani kwao Ujerumani ambayo aliisaidia kutwaa ubingwa wa ligi ya Ujerumani Bundesliga.
Thomas pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mashindano ya kombe la dunia na kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 ambako alicheza mechi zote za hatua ya mtoano kuanzia robo fainali, nusu fainali na fainali.
thomas 2Kiungo huyu mshambuliaji pamoja na kuwa raia wa Ujerumani alichea sehemu kubwa ya soka lake nchini England kwenye timu za Aston Villa, West Ham United na Everton ambapo pamoja na Stuttgart, Bayern Munich ndiko alikoanzia soka lake na Werder Bremen.
Moja ya vitu ambavyo Hitzlsperger atakumbukwa navyo ni mashuti makali aliyokuwa anapiga kwa mguu wake wa kushoto na alifunga mabao mengi sana kwa style hiyo kabla ya kustaafu soka mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 31 baada ya kuandamwa na majeraha tofauti ya goti kwa muda mrefu.
thomas 3Thomas Hitzlsperger anakuwa mchezaji wa pili maarufu kujitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja baada ya mchezaji wa zamani wa Leeds United Robbie Rogers ambaye kwa sasa anacheza kwenye klabu ya Los Angeles Galaxy naye kujitangaza kuwa shoga.

ZITTO ASHINDAKESI DHIDI YA CHADEMA MAHAKAMA KUU...MATUKIO KATIKA PICHA

Zitto Kabwe akipeana mikono na Wakili wa CHADEMA,Tundu Lisu baada ya kukibwaga chake chake.
 Wakili wa chama cha CHADEMA,Mh Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje ya Mahakama kuu Kanda ya Dar Es Salam juu ya maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama chake.
 Tundu Lisu akiwatuliza na  kuwasihi wafuasi wa chama chake CHADEMA kutokufanya fujo na badala yake waondoke eneo hilo kwa utulivu na amani.Nje Mahakama makundi ya wafuasi wa CHADEMA na Zitto Kabwe walikuwa wakirushiana mawe kiasi hata mmoja wa wafuasi wa CHADEMA kujeruhiwa kichwani kwa jiwe.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amekibwaga chama chake,kufuatia  Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.

Aidha Wakili wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na maamuziki ya Mahakama,hivyo akabanisha kuwa  Zitto Kabwe atabaki kuwa Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una  muda wake basi tujipe muda tuu..alibainisha Tundu Lisu.

TAARIFA JUU YA MWANAMKE ALIYEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DARESALAAM HAPO JANA AKIPELEKA NCHINI CHINA

Mwanamke mmoja  Salma Omari Mzale, alikamatwa Airport Dar es Salaam na Madawa ya Kulevya, akielekea nchini China. Mpaka sasa ameshikiliwa na Polisi wa usalama kitengo cha madawa ya kulevya cha uwanja wa ndege. Mwanamke huyo mkazi wa Mbagala Kongowe, anaendelea kutoa kete hizo katika vyoo vya Uwanja wa Ndege. Hadi saa 1 jioni (mida ya Tanzania). Uchunguzi wa kina unaendelea.
Habari kamili itawajia hivi punde.

TASWIRA YA HALI ILIVYOKUWA JANA MAHAKAMANI KWENYE KESI YA ZITTO KABWE NA CHADEMA..TAZAMA PICHA HAPA

Wafuasi hao wakianza kuzichapa kavu kavu nje ya Mahakama hiyo.
Baadhi ya wafuasi wa Zitto, wakiwa na mabango nje ya Mahakama hiyo leo mchana.


Mmoja wa kijana aliyekamatwa na askari baada ya kuleta fujo eneo la mahakama.

Wanausalama wakipanga mikakati ya kuimarisha ulinzi eneo la Mahaka
ma Kuu jijini Dar.

Mfuasi wa Zutto akiwa na bendera ya CHADEMA


Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Dar es Salaam, SACP Marietha Minangi, wakati akiwasili Viwanja vya Mahakama Kuu.

Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwahutubia wananchi waliofika mahakamani hapo baada ya hukumu ya Zitto kuahirishwa mpaka kesho saa nane mchana. .

Mwanasheria wa Zitto Kabwe, Albert Msando (kushoto) akitoka mahakamani baada ya hukumu kuahirishwa.

Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo wananchi eneo la Mahakama Kuu.

 
Design by Jambo Tz