MCHEZAJI WA BAYERN MUNICH NA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI AJITANGAZA KUWA SHOGA

thomas 1Nyota wa zamani wa Ujerumani Thomas Hitzlsperger aliyeanzia soka lake kwenye klabu ya Bayern Munich  amejitangaza kuwa shoga.
Aliwahi kucheza kwenye ligi ya England kwa muda wa miaka mitano akicheza kwenye klabu ya Aston Villa kabla ya kujiunga na VFL Stutgart ya nyumbani kwao Ujerumani ambayo aliisaidia kutwaa ubingwa wa ligi ya Ujerumani Bundesliga.
Thomas pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mashindano ya kombe la dunia na kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2008 ambako alicheza mechi zote za hatua ya mtoano kuanzia robo fainali, nusu fainali na fainali.
thomas 2Kiungo huyu mshambuliaji pamoja na kuwa raia wa Ujerumani alichea sehemu kubwa ya soka lake nchini England kwenye timu za Aston Villa, West Ham United na Everton ambapo pamoja na Stuttgart, Bayern Munich ndiko alikoanzia soka lake na Werder Bremen.
Moja ya vitu ambavyo Hitzlsperger atakumbukwa navyo ni mashuti makali aliyokuwa anapiga kwa mguu wake wa kushoto na alifunga mabao mengi sana kwa style hiyo kabla ya kustaafu soka mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 31 baada ya kuandamwa na majeraha tofauti ya goti kwa muda mrefu.
thomas 3Thomas Hitzlsperger anakuwa mchezaji wa pili maarufu kujitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja baada ya mchezaji wa zamani wa Leeds United Robbie Rogers ambaye kwa sasa anacheza kwenye klabu ya Los Angeles Galaxy naye kujitangaza kuwa shoga.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz