
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa
Tanzania amewafukuza kazi mawaziri wanne baada ya kutengua uteuzi wao
kwa tuhuma za kushindwa kusimamia operesheni ya kuwasaka majangili.
Hatua hii
ya Rais Kikwete ya kutengua uteuzi unatokana na shinikizo la Bunge la
Tanzania ambao walitaka mawaziri hao wajiuzulu wenyewe au rais awafukuze
kazi kutokana matukio ya mauaji, utesaji na uvunjifu wa haki za
binadamu wakati wa operesheni hiyo uliofanywa na watendaji walio ndani
ya wizara zao., utesaji na ukiukaji wa haki za binadamu wakati
operesheni ulifichuliwa na taarifa ya kamati ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na utalii iliyopewa jukumu ya kufanya uchunguzi baada ya
kuwepo kwa malalamiko kuwa operesheni hiyo uliambatana na ukiukaji wa
haki za binadamu.
Miongoni
mwa mateso na ukiukwaji wa haki za binadamu uliotajwa kwenye ripoti ya
kamati hiyo ilikuwa ni mauaji, utesaji ikiwemo kuwalazimisha baadhi ya
wanaume kufanya mapenzi na miti au wanyama waliokufa.

Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda Akisoma
Uwamuzi huo Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda Amesema amewasiliana na Rais
Kikwete Ambaye Yupo Nje ya Nchi Kwa Matibabu ameridhia Mawaziri hao
kuachia ngazi.Mawazi walioachishwa kazi ni Waziri wa Mambo ya Ndani,Dr Emmanuel,Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa. Mh Shamsi Nahodha,Waziri wa Maliasili na Utalii Mh Balozi Kagasheki,Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Dk David Mathayo..
Waziri wa Mambo ya Ndani,Dr Emmanuel


Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii

Waziri wa Mifugo na Uvuvi

0 comments:
Post a Comment