skip to main |
skip to sidebar
Ndoa ya mastaa wa filamu, Mike Sangu na Ndumbagwe
Misayo ‘Thea’ imevurugika baada ya kutokea hali ya kuzinguana kwa wawili
hao chanzo kikidaiwa ni kukosekana uaminifu.
Chanzo cha habari hii ambacho ni rafiki wa Thea kilieleza kuwa,
kutibuana kwa wanandoa hao kumekua kufuatia Thea kuhisi mwenzake
anamzunguka.“Kimsingi hali si shwari, ndoa inawaka moto, Thea anamtuhumu
Mike kuwa anamsaliti, chanzo ni hizi simu na siku hiyo mtiti
ulipotokea, shosti alikwenda kwao na mpaka leo hii (Juzi Jumatato)
anasubiri wasuluhishwe,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo, Mike alitafutwa na alipoulizwa kuhusu
ndoa yake kutibuka alisema: “Mh! Watu ni wambeya sana mimi na mke wangu
tulitokea kutoelewana na si mambo ya meseji wala wanawake, mimi sina
mambo hayo kabisa, siwezi kuongelea mambo mengi mpaka nitakapoenda
nyumbani kwa mke wangu lakini kilichotokea ni cha kawaida tu .”Thea
hakuweza kupatika kuzungumzia ishu hiyo.
0 comments:
Post a Comment