HISTORIA FUPI YA MAREHEMU ISAAC ABRAHAMU SEPETU AMBAYE NI BABA YAKE MZAZI WEMA SEPETU.

 
Balozi Isaac Abraham Sepetu alizaliwa October 15, 1943, ni mzaliwa wa Tabora ila alikulia Zanzibar na alikuwa ni mkaazi wa Zanzibar mpaka mauti yanamfika
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu alipata elimu yake ya msingi na sekondari  katika shule ya St.joseph’s  kwa sasa inaitwa Tumekuja huko Zanzibar mnamo mwaka 1952 hadi 1963, vilevile aliweza kujiunga na chuo kikuu huko Berlin nchini Ujerumani mwaka 1964 hadi 1970 alisomea Shahada ya Uchumi,
Marehemu alikuwa anauwezo wa kuongea lugha tatu (3) kwa ufasaha ambazo ni ;- kiswahili, kingereza  na kijerumani.

KAZI
Alianza kufanya kazi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 1971 hadi 1972 kama Mkuu wa Bizanje Msaidizi na pia alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ikulu. Baada ya hapo mwaka 1972 hadi 1977 alikuwa Naibu Waziri Mambo ya Nje  katika serikali ya Muungano Zanzibar, mnamo mwaka 1977 hadi 1979 Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu  alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji, Ilipofika mwaka 1979 hadi 1982 alikuwa Waziri wa Utalii na Maliasili .
Marehemu Balozi  Sepetu mwaka 1982 hadi 1989 alipewa nafasi ya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Moscow na mwaka 1989 hadi 1990 alikuwa Balozi wa nchi ya Zaire, Kinshasa

Katika Serikali ya Mapinduzi
Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Waziri wa Nchi, Mipango pia alikuwa Mshauri wa Rais, Ushirikiano wa Kimataifa na pia alikuwa Katibu , Kamati ya Pamoja(IPC) CCM/CUF, Zanzibar Mwaka 2001 hadi 2005 alikuwa mbunge wa bunge la Afrika ya Mashariki

Uzoefu wa Kisiasa
Mwaka 1977 hadi 2005 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz