Kwa
mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lililoongeza faraja na furaha ya
shetani kule kuzimu, lilijiri juzikati huko Kimara Mwisho ndani ya
gesti moja (jina lipo kwenye droo zetu).
ALIYENASA AANZA KUMWAGIKA
Akizungumza
kwa uchungu mkubwa, mume wa mwanamke huyo ambaye hakupenda jina lake
liupambe ukurasa huu, alisema siku nyingi Manfree amekuwa akimsumbua
mke wake, hali iliyokuwa ikimpa wakati mgumu mwanamme huyo mwenye mke.
“Jamaa
amekuwa akimsumbua sana mke wangu, nilipokuja kuzipata taarifa hizi
nilishangaa sana lakini pia niliumia kama mwanamme,” alisema mwenye mke
huyo.
MAZOEA YALIPOANZA

Kwa
mujibu wa mume huyo, kufahamiana kwa Manfree na mkewe kulikolea zaidi
baada ya mwanamke huyo kuhitaji fremu kwa ajili ya biashara ya duka
ambapo kwa kutumia uenyeji wa jamaa huyo, alionesha kutaka kumsaidia.
SINEMA YA KUNASWA ILIPOANZA
Mwanamme
huyo aliendelea kusema kuwa sinema ya kunaswa kwa mwanamme huyo
ilianza siku moja baada ya yeye kwenda kwenye baa ya jamaa huyo
kuangalia mpira (hakuzitaja timu).
Alisema
akiwa hapo baa, mara mke wake alitokea na kukaa kwenye kiti, meza
nyingine. Jamaa huyo naye akaenda kukaa na mke wa jamaa na kuanza
kuzungumza.
“Mimi
sikujua walichokuwa wakikizungumza na wala sikuwa na wasiwasi kwa vile
jamaa ananifahamu, anafahamu yule ni mke wangu na anawafahamu hadi
watoto wangu,” alisema mwanamme huyo.
Akaongeza:
“Tulipofika nyumbani, mke wangu akasema amesikia mimi nina wanawake
wengi nje, nimewafungulia biashara na mambo mengine kibao.
“Nilimuuliza
ameambiwa na nani, akawa anagomagoma kunijibu lakini nilipombana sana
mwisho akamtaja jamaa. Kumbe alipokaa naye pale baa ndiyo alikuwa
akimwambia uongo huo.
“Mke
wangu akaongeza kusema kuwa jamaa huyo kwa muda mrefu amekuwa akimtaka
wakutane ‘praiveti’ lakini yeye amekuwa akimkatalia kwa sababu
analinda heshima ya ndoa yake.
“Mke
wangu alinionesha meseji ambazo jamaa alikuwa akimtumia, niliumia
sana. Kwa kweli inauma sana jamani hasa kitendo hicho kufanywa na mtu
ambaye mnafahamiana!”
MTIRIRIKO UNAENDELEA
Kwa mujibu wa mwanamme huyo, hali hiyo iliendelea kuisumbua ndoa yake huku maneno ya Manfree yakizidi kumvuruga kichwani.
SINEMA KAMILI HII HAPA SASA
Mume
huyo alizidi kueleza kuwa baada ya mkewe kukiri kwamba Manfree amekuwa
akimtaka wakutane chemba ndipo kwa pamoja walikubaliana kuandaa
fumanizi.
“Nilimwambia
mke wangu lazima tutege fumanizi, lengo ni kumfanya jamaa aachane na
tabia hizi ambazo zinaweza kuharibu ndoa, watoto wakateseka na mambo
menginemengine. Nilimruhusu amkubalie kukutana gesti,” alisema mume.
PICHA LINAKOLEA
Mume
anasema siku ya tukio, Manfree bila kujijua alimtumia meseji mwanamke
huyo, akamuomba wakutane ndani ya gesti moja iliyopo Kimara Mwisho
ambapo bila kupoteza muda mwanamke huyo alimtonya mumewe juu ya meseji
hiyo.
“Baada ya kunionesha meseji hiyo nilitafuta baadhi ya marafiki zangu ili twende pamoja kwenye eneo la tukio wakawe mashahidi.”
UTAMU ZAIDI
Baada
ya mke kufika ndani ya gesti hiyo, mume anadai alimtaarifu jamaa huyo
ambaye alitokea na kumwambia mwanamke huyo kuwa amuongezee shilingi
elfu kumi kwani chumba ni elfu ishirini.
CHUMBANI ZAIDI
Kwa
mujibu wa mume huyo, baada ya wawili hao kuingia chumbani humo, jamaa
huyo alivua nguo zote na kukimbilia bafuni. Nyuma, mwanamke huyo
aliutumia mwanya huo kumtaarifu mumewe ambaye naye aliwashika masikio
marafiki ili wakae mkao wa kumnasa jamaa huyo.
Muda
mfupi baadaye, mume anasema Manfree alitoka bafuni na kufikia
kitandani puu! Hana hili wala lile, mwanamme huyo akiwa na ‘skwadi’
yake walizama ndani, wakagonga mlango, Manfree akakaribisha, alijua ni
mhudumu amemletea bia maana aliagiza.
Mume
alizidi kusema kuwa jamaa alipigwa butwaa na kuonekana kuweweseka.
Yeye akamuuliza imekuaje yuko na mke wake chumbani? Jamaa akawa hana la
kujibu.
MAELEZO YA KWENYE VIDEO
Katika
maelezo yaliyomo kwenye video ya tukio zima (ipo chumba cha habari
Global), Manfree anajieleza akimuomba msamaha mume huyo pamoja na wote
waliokuwa chumbani humo.
MKE WA MANFREE AITWA
Mwanaume
huyo anadai kuwa kwa hasira aliamua kumpigia simu mke wa Manfree ili
afike kwenye gesti hiyo kushuhudia mumewe alivyokutwa na mke wa mtu
gesti.
Anasema: “Mke alifika, akamkuta mumewe hajavaa nguo, aliumia sana lakini hakuwa na la kufanya.”
JAMAA KIZIMBANI
Baada
ya ‘mhangaikaji’ wetu kuzipata data hizo, juzi asubuhi alimtafuta
Manfree kwa njia ya simu ya mkononi kupitia namba alizopewa na watu wa
karibu. Mwanzoni jamaa huyo alionekana kugoma lakini baada ya kubanwa
kwa vielelezo alikubali huku akisema japo alinaswa lakini pia jamaa hao
walitumia njia za kumteka.
“Aa..!
Ni kweli nilikutwa na zahama hiyo lakini jamaa waliniteka bwana. Hata
hivyo, sitarudia tena kuwa na uhusiano na wake za watu na
tulishamalizana na mwenye mke kwa kumuomba msamaha,” alisema Manfree.
MKE WA MANFREE
Katika
hali ya kushangaza, baada ya mkewe kupigiwa simu na mwandishi na
kukiri kuwa ni kweli mumewe alinaswa chumba cha gesti akiwa na mke wa
mtu, alisema bado anampenda na kwamba ndoa yao bado iko imara kama
mizizi ya mti wa mbuyu!
“Ni
kweli mume wangu alifumaniwa lakini bado nampenda sana na siwezi
kumwacha, nitamvumilia maana ni mume wangu,” alisema mke wa Manfree
aliyejitambulisha kwa jina moja la Sarah.
(Maneno yaliyotumika kwenye picha za ukurasa wa mbele, ni kama wanasema na si maneno halisi.)
0 comments:
Post a Comment