WALIO MUUA BILIONEA ERASTO MSUYA WAKUTWA KWA MGANGA WAKIFANYIWA ZINDIKO

Jeshi la polisi mkoa wa kilimanjaro linawashikilia watu wanne zaidi wakidaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara bilionea wa madini ya tanzanite Arusha Erasto Msuya 43 wawili kati yao walikutwa kwa mganga wa kienyeji (sangoma) wakifanyiwa zindiko ili wasikamatwe na vyombo vya dola.

Pia jeshi limenikiwa kunasa bunduki aina ya SMG yenye namba za usajili KJ10520,inayoaminika kutumika katika mauaji hayo.Msuya aliuawa kwa kupingwa risasi zaidi ya 10 kifuani Augost 7mwaka huu,katika eneo la mijohoroni wilayani Hai.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Robert Boaz aliwataja watuhumiwa kuwa ni Sadiki Jabiri 32 mkazi wa Dar es Salaam na Lang'angata wilayani Hai

.Karimu Kihundwa 33 mkazi wa Lawate Wilayni Siha ambao wanatajwa kuwa ni muhimu katika mauji hayo.Alisema watuhumiwa hao wawili walikamatwa eneo la Kaliua sikonge mkoani Tabora wakiwa kwa sangoma wakifanyiwa zindiko ili wasitiwe mbaroni.

Baada ya kuhojiwa na polisi walieleza jinsi walivyoshiriki mauaji hayo na mahali walipoficha silaha hiyo na pikipiki zilizotumika katika tukio hilo.

Boaz aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Jalila saidi 28 mkazi wa Mkoani Manyara na Kondoa Mkoani Dodoma na Joseph Damas Mwakipesile maarufu kam (chusa )35 ambae pia ni mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite anayeishi Arusha .

Alisema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata pikipiki nyingine inayodaiwa kutumika katika tukio hilo yenye uasjili T751 aina ya Kinglion rangi nyeusi ambayo wakati wa tukio ilikuwa ikutumia namba za bandia.

Kamanda Boaz alisema bunduki iliyokamatwa ilikutwa ikiwa imefichwa kwenye tindiga katika eneo la Baroi kwenye mpaka wa wilaya ya Hai na Siha.

Kukamwatwa kwa watuhumiwa hao wanne sasa kunabadilisha sura ya kesi hiyo ambapo awali walifikishwa mahakani watuhumiwa watatu Sharifu Athumani (31),Shaibu Saidi maarufu kama mredi (38) na Mussa Mangu (30) Kesi huyo namba 6 ya mwaka2013,imepangwa kesho tehehe 18,09,2013 kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.

Source:Tanzania Daima



0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz