DENTI AMCHOMA KISU BABA YAKE KWENYE PAJI LA USO KISA NGONO

 
DENTI wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo (jina tunalo) iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha, anadaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba yake mzazi Daudi Msemo baada ya kuonywa kuachana na tabia ya kuchanganya ngono na masomo.

Hayo yamesemwa na Fatuma Daudi ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi huyo mara baada kutokea tukio hilo la kusikitisha hivi karibuni nyumbani kwao Monduli ambapo denti alipofikishwa polisi alisema alifanya kitendo hicho kwa sababu baba yake alitaka kumbaka.

“Binti yetu huyu amekuwa akibadilika tabia na mara nyingi tumekuwa tukimuonya aache vitendo vya umalaya akiwa mwanafunzi lakini bado amekuwa akiendeleza tabia yake hiyo ambayo sisi wazazi tumeona ni kudharau maagizo yetu,” alisema Fatuna.

Aliongeza kuwa, tabia hiyo ilikuwa ikimfanya mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kutorudi kabisa.

Mama huyo alisema, kutokana na tabia hiyo waliamua kumdhibiti ili aache lakini matokeo yake alimchoma kisu baba yake na akamsingizia alitaka kumbaka hali iliyowalazimisha polisi kuwaweka ndani wote.

Fatuma alikwenda mbali zaidi kwa kuwaomba baadhi ya wanajeshi ambao wana uhusiano wa kimapenzi na binti huyo waache kwa kuwa ni kinyume cha maadili na mwanaye bado ni mwanafunzi wa kidato cha nne.

Maelezo ya denti huyo yalimfanya baba mzazi kuahidi kujiua baada ya kutoka kituoni hapo akidai amedhalilishwa sana, hali iliyowafanya polisi kuamua kuendelea kumshikilia licha ya kwamba walishamruhusu kutoka baada ya mkewe kumtetea.

Afisa mmoja wa jeshi la polisi ambaye hakutaka kuandikwa jina lake kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

“Tunaendelea na uchunguzi na wote wawili, baba na mwanaye tunawashikilia ili kubaini chanzo cha kutokea kwa tukio hilo, baada ya uchunguzi maelezo zaidi utapewa na kamanda wa mkoa afande Liberatus Sabas, kwani ndiye msemaji wa jeshi mkoani hapa,” alisema afisa huyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz