UWOYA ALIA NA SHIGONGO KWA KUMCHAFULIA KUWA YEYE NI MWIZI WA SIMU IPHONE-5

Ukurasa wa mbele wa gazeti la Risasi la leo Jumamosi (Sept 14) umetawaliwa na habari inayomhusu msanii wa Bongo Movie Irene Uwoya yenye kichwa cha habari “UWOYA MBARONI KWA WIZI WA SIMU!!”.


“MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.

MAMBO yanaendelea kumwendea kombo mwigizaji huyo huku akiwa ameanza kuporomoka vibaya kwenye sanaa na kujikuta akiingia matatani kwa tuhuma za aibu.

Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.”

Katika kujibu tuhuma zilizoripotiwa na gazeti hilo, Uwoya kupitia akaunti yake ya Instagram leo amepost picha ya ukurasa wa mbele wa gazeti hilo wenye habari hiyo pamoja na maneno yafuatayo:


“Minimti wenye matunda milele siogop kupigwa mawe…shigongo kamua kunichafua coz nakes nae mahakaman…anadhan ntaiacha never yeye aponde anavyoweza ila mwisho wasiku sheria iatafata mkondo wake….minayake mengi nayajua ila ngoja ninyamaze nisimwagiwe tindikali”

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz