Baada
ya kukamatwa mama huyo katili alkabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia
na watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU akimjulia
hali mtoto Emilly
Wimbi
la ukatili dhidi ya watoto bado limezidi kuchukua sura mpya baada ya
mtoto EMILLY GEORGE[7] Mkazi wa kijiji cha RUANDA wilaya ya Mbeya
kuunguzwa vibaya mikono yote miwili na mama yake mzazi ELESIA
MWASILE[41] kwa maji ya moto kisha kufungiwa ndani kwa siku saba bila
matibabu yoyote.
Akiongea
huku akitetemeka kwa hofu ELESIA amesema kuwa chanzo cha cha kumchoma
mtoto huyo ni kutokana na malalamiko ya majirani wakimtuhumu mtoto huyo
kujihusisha na vitendo vya wizi vikiwemo wizi wa pesa na mayai ya kuku.
Tukio
la mwisho lililopelekea mtoto huyo hadi kuchomwa ni pale ilipodaiwa na
mama huyo kuwa mtoto aliiba mayai akidai amechoshwa na tabia za
malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa jirani zake.
Baada ya kuunguzwa kikatili mtoto huyo alifungiwa ndani kwa siku saba bila
matibabu yoyote hali iliyowafanya majirani kuuliza aliko mtoto kutokana
na mtoto huyo kutoonekana mitaani hali iliyopelekea kutolewa taarifa
ofisi ya kijiji ili kubaini aliko mtoto.
Uongozi
wa kijiji baada ya kupata taarifa kwa majirani walifanya upekuzi na
kumkuta mtoto amefungiwa ndani huku akiwa na majeraha makubwa katika
mikono yote miwili ndipo taarifa ilitolewa kituo cha Polisi MBALIZI
ambapo mama huyo alikamatwa.
Baada
ya kukamatwa mama huyo katili alkabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia
na watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU na
Mwenyekiti MARY GUMBO ambaye muda wote alikuwa akiangua kilio kutokana
na kitendo alichofanyiwa mtoto na mama yake mzazi.
Hivi
sasa mwanamke huyo anahojiwa na Polisi kituo kikuu cha kati na
atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na mtoto amelazwa katika
Hospitali ya Rufaa wadi namba tano akiendelea kupatiwa matibabu.
Vitendo
vya unyanyasaji vimendelea kukemewa Mkoani Mbeya na Asasi mbalimbali
hasa kwa watoto vikiwemo vya ubakwaji,ulawiti,kazi za ndani na baadhi ya
watoto wamepata ulemavu wa kudumu ikiwemo kupoteza viungo.
N.B:PICHA NI MBAYA SANA NDIO MAANA HATUJAZIWEKA ILA KWA MAAMUZI YAKO MWENYEWE UNAWEZA ANGALIA KWA KUBOFYA BAPO CHINI
|
0 comments:
Post a Comment