Zitto Kabwe akipeana mikono na Wakili wa CHADEMA,Tundu Lisu baada ya kukibwaga chake chake.
Wakili
wa chama cha CHADEMA,Mh Tundu Lisu akizungumza na vyombo vya habari nje
ya Mahakama kuu Kanda ya Dar Es Salam juu ya maamuzi yaliyotolewa na
mahakama hiyo kuhusiana na kesi ya Zito Kabwe dhidi ya chama chake.
Tundu
Lisu akiwatuliza na kuwasihi wafuasi wa chama chake CHADEMA
kutokufanya fujo na badala yake waondoke eneo hilo kwa utulivu na
amani.Nje Mahakama makundi ya wafuasi wa CHADEMA na Zitto Kabwe walikuwa
wakirushiana mawe kiasi hata mmoja wa wafuasi wa CHADEMA kujeruhiwa
kichwani kwa jiwe.
Naibu
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amekibwaga chama chake,kufuatia
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa,
kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya
Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho
itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza
kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.
Aidha
Wakili wa chama cha CHADEMA,Tundu Lisu ameeleza kutoridhika na
maamuziki ya Mahakama,hivyo akabanisha kuwa Zitto Kabwe atabaki kuwa
Mbunge wa Mahakama,na kama tujuavyo Mbunge wa Mahakama una muda wake
basi tujipe muda tuu..alibainisha Tundu Lisu.

0 comments:
Post a Comment