MH. MKONO KUMPATIA MH. ZITTO MAGARI MAWILI
Nimesikitishwa
na jinsi Chama kikuu cha upinzani ambavyo kwa siku za hivi karibuni
kimeingia katika migogoro ambayo inaathari kubwa kwa ustawi wa
demokrasia hapa nchini.
Nimesoma
kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mimi Mh. (Nimrod Mkono) kumpatia
Zitto Kabwe (MB) magari mawili (Land Cruiser pamoja na Nissan Patrol).
Kwanza napenda ifahamike
kwamba sijawahi kumpatia Zitto magari. Isipokuwa kuhusu hiyo Land
Cruiser; nilitoa msaada wa kuwanusuru kule Tarime kwenye msiba wa
marehemu Chacha Zakayo Wangwe (MB) Tarime. Wakiwa wanatishiwa kupigwa
(Freeman Mbowe pamoja na Zitto Kabwe) nilijitolea gari langu lenye
bendera ya Bunge, liwachukuwe na kuwapeleka Mwanza wakiwa salama, na
ilifanyika hivyo.
Baada ya kufika Mwanza, Mhe.
Zitto aliwasiliana na mimi, kuhusu ununuzi wa gari hilo, nami kupitia
kwa wakala wangu Africariers; nilimuuzia Zitto hilo gari.
Kuhusu hilo gari la pili:
(Nissan patrol) Mhe. Zitto Kabwe alilikodi, na mpaka sasa anaendelea
kulipa vizuri tu; lakini pia ifahamike kwamba hata nyaraka za gari hilo
bado ninazo mimi kama mmiliki halali na sijawahi kuhamisha umiliki wake
(Transfer of ownership)
KUHUSU KUTOA FEDHA KWA CHADEMA
Nimesikitishwa na ninataka
kuweka wazi kwamba, sijawahi kuongea na Tundu Lissu kama inavyodaiwa kwa
masuala yoyote binafsi isipokuwa tukiwa kwenye kamati ya Katiba na
Sheria.
Ikumbukwe kwamba, nimepita
bila kupingwa kwa vipindi vitatu mfululizo (2000, 2005 na 2010). Ni
historia ya aina yake; lakini pia uchapakazi wangu kwenye jimbo la
Musoma vijijini. Ushindi wangu wa kupita bila kupingwa kwa kiwango
kikubwa umekuwa unatokana na bila shaka umahiri wangu kwa kufanya kazi
za wananchi kwa kiwango kikubwa.
0 comments:
Post a Comment