Wananchi wakiwa wakitafakari nje ya jengo la Kanisa la Gilgal Christian Centre lililopo Pasiansi Ilemela jijini Mwanza.
----------
Mtu mmoja ameuawa na
wengine watatu kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililofanywa na kundi la watu
wasiofahamika usiku wa kuamkia jana katika kanisa la Gilgal Christian Worship
Centre lililopo eneo la Pasiansi wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Mwanza , Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mpaka sasa
hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa, hali ambayo
inalifanya tukio hilo kuwa na maswali mengi likihofiwa kufananishwa na yale ya
uchomaji moto Makanisa.
Waumini wakitafakari tukio hilo la uvamizi lililosababisha taharuki kwa wakazi wa jiji la Mwanza.Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza
Askofu wa kanisa la Gilgal Christian Centre Eliabu Sentozi.
Tukio hilo lililotokea
majira ya saa saba usiku linamtaja Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi na ni
mwenyekiti wa vijana wa kanisa kuuawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini
wengine Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu ambao hali zao zinatajwa kuwa taabani
wakipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza baada ya kujeruhiwa
vibaya kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao.
Askofu wa kanisa hilo
Eliabu Sentoz amelaani tukio hilo akilitaja kuwa ni la kinyama kwani
limefanyika sehemu ya ibada akiwataka wananchi kuungana pamoja kulisaidia jeshi
la polisi katika kutoa taarifa kuwabaini wahusika wa shambulio hilo na
akaiomba serikali kuongeza nguvu kukabiriana na wahalifu hao.
0 comments:
Post a Comment