WATUHUMIWA MADAWA YA KULEVYA WAONYESHA JEURI MAHAKAMANI

.


Watuhumiwa wa madawa ya kulevya wakiwa wameficha nyuso zao katika Mahakama Kuu jijini Dar leo.
 
 Mmoja wa watuhumiwa akiwa ameinamisha kichwa chake kukwepa kamera za wanahabari. Askari Magereza akimtia pingu mtuhumiwa katika kesi ya madawa ya kulevya. Watuhumiwa wakificha sura zao kwa wanahabari waliokuwa na hamu ya kupata picha zao.
HALI ya sintofahamu imetokea leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam wakati Jaji Mwakipesile alipomaliza kusikiliza kesi inayowakabili watuhumiwa wa madawa ya kulevya. Waandishi wa habari waliwakaribia watuhumiwa hao ili kuwapiga picha ndipo walipowakwida baadhi yao na wengine wakiwa 'busy' kuficha nyuso zao kwa kile walichodai kutotaka kupigwa picha wala kutolewa kwenye vyombo vya habari. Aidha baadhi yao walitinga kortini wakiwa wamevalia 'Ki-ninja' (wakiwa wameficha sura zao zisifotolewe) hali iliyozua mtafaruku kortini hapo, kabla ya polisi kuwapiga pingu kuwarudisha rumande. Baada ya jaji kuahirisha kesi hiyo, baadhi ya watuhumiwa walikuwa mbogo huku mmoja wao akimtupia teke mpigapicha hali iliyoonesha hakutaka kabisa kuchukuliwa picha na waandishi





0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz