Padri Joseph Magamba wa Kanisa
Katoliki Parokia ya Machui Zanzibar aliyemwagiwa tindikali akisaidiwa
kushuka kwenye ndege na Padri Thomas Assenga(kushoto) wa Kanisa la
Mtakatifu Joseph Zanzibar baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Julius
Nyerere Dar es Salaam jana kuelekea katika hospitali ya Taifa Muhimbili
kwa matibabu zaidi.Picha na Fidelis Felix
DAR/ZANZIBAR.
SIKU moja baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang’amba kumw
agiwa tindikali na watu wasiojulikana, imebainika kuwa alitishiwa kuuawa miezi mitatu kabla ya kukutwa na tukio hilo.
Wakati
Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,
ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini
na serikali visiwani humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku
akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo.
Kiongozi
huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada
ya kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya
Shirika la Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye
kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Dk
Shein alisema Polisi inatakiwa kuongeza nguvu za uchunguzi ili
kukabiliana na matukio ya kikatili ya umwagaji wa tindikali,
yanayoshamili visiwani humo hivi sasa.
“Hatuwezi
kuviacha vitendo hivi viendelee … ni lazima Jeshi la Polisi lijitahidi
kuwatafuta wahusika ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Dk Shein.
Dk
Sheni alisema, kitendo hicho ni cha kikatili na kisichovumilika na
kuongeza kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa
upande wake, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas
Assenga aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma
Padri Mwang’amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati
akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.
Alisema
kabla ya kufika kituoni hapo, kuna eneo ambalo nyakati za asubuhi watu
hufanya mazoezi barabarani ambapo kuna mtu mmoja alimtolea maneno ya
vitisho.
“Unajua
kawaida ya watu wa Zanzibar hufanya mazoezi barabarani, sasa kipindi
anapita eneo hilo katika kilima, kuna mtu alimwambia atamfanyia kitu
kibaya ambacho hatujui ndiyo hiki au la,” alisema Padri Assenga na
kuongeza:
Alisema Juni mwaka huu mara baada ya kupewa vitisho hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa Sheha wa eneo hilo na kituo cha polisi.
“Mara
baada ya kutolewa vitisho hivyo Juni mwaka huu, alichukua jukumu la
kwenda kutoa taarifa kwa mkuu wa eneo hilo (Sheha) na kituo cha polisi.”
Akielezea
tukio la kumwagiwa tindikali Padri Mwang’amba, alisema alimwagiwa saa
9:45 alasiri juzi wakati akizungumza na simu nje ya internet café
iliyopo eneo la Mlandege. -MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment