MWANAMKE ANUSULIKA KUUWAWA BAADA YA KUTAKA KUIBA MTOTO HUKO MUSOMA...


 MWANAMKE ALIOFEFAHAMIKA KWA JINA LA ZAWADI AKIWA KITUO CHA POLISI  STEND MJINI MUSOMA                                                      

 WANANCHI WAKITAFAKARI KUTOKANA NA TUKIO HILO
 NJE YA KITUO CHA POLISI                                            
 MTOTO WA SIKU MOJA ALIYENUSULIKA KUIBWA                                        
 NI ULINZI MKALI KWA MTUHUMIWA
MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Zawadi Hamisi(22) mkazi wa Butimba mkoani Mwanza amenusulika kuuwawa na Wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuiba mtoto mchanga wa siku moja kwenye hospitali ya mkoa wa Mara.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 mchana maeneo ya barabara ya sokoni Manispaa ya Musoma baada ya mwanamke huyo kumdanganya mzazi wa mtoto huyo kuwa anaitwa na mama yake na kutumia mwanya huo kuondoka na mtoto huyo kabla ya kusaidiwa na wasamalia wema kumkamata Mwanamke huyo.

Akizungumza na Habari leo katika kituo kidogo cha polisi cha stedi ya zamani mjini hapa huku akibubujikwa na machozi,mzazi wa mtoto huyo Angelina Singu(22) mkazi wa kijiji cha Masurura Wilayani Butiama alisema mwanamke aliyedaiwa kumuiba mtoto huyo mwenye jinsia ya kiume alimwambia mama yake yupo stend anamsubilia ili waondoke.

Alisema alimfata akiwa hospitali ya mkoa wa Mara akijiandaa kuondoka baada ya kujifungua septemba septemba 19 na kumueleza mama yake anamuita na kumtaka msaidie mtoto ili waweze kumfuata na kuondoka kurudi nyumbani.

Angelina alisema baada ya kutoka nje ya geti la hospitali ya walitembea hadi sted ya zamani na baadae wakiwa umbali kidogo kutokana na mwendo wake kuwa mdogo kutokana na uzazi alimuona mwanamke huyo akipanda pikipiki maarufu kama bodaboda na kuanza kuondoka huku akimuacha.

Alisema baada ya kuona hali hiyo aliamua kupiga kelele ya kuomba msaada ndipo wasamalia wema pamoja na baadhi ya waendesha pikipiki walipoamua kuifukuza pikipiki aliyopanda mwanamke huyo pamoja na mtoto aliyeibwa na kufanikiwa kumkamata barabara ya sokoni.

"Inaonekana huyu mwanamke alinifatilia pale hospitalini tangu nilipojifungua,hakuwa na nia njema ni kweli alitaka kuondoka na mtoto wangu....masikini nimeangaika miei tisa leo mtoto wangu anataka kuchukuliwa kwa kweli nawashukuru walionisaidia ningekuwa kwenye hali gani mimi.

"Wanawake tuoneane huruma hili sio jambo jema hivi karibuni nilisikia kwenye vyombo vya habari mkoa mmoja kuna Mwanamke kaiba mtoto kumbe mambo haya yapo imeniuma sana na namshukuru mungu na walionisaidia jambo hili na vyombo vya sheria vichukue hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizi"alisema Angelina.

Mwanamke anayedaiwa kufanya jaribio la kuiba mtoto huyo alisema alitoka Mwanza kuja Musoma kwa ajili ya kumsalimia kaka yake na alikwenda hospitali ya mkoa wa Mara kuchukua dawa kwa ajili ya matibabu.

Alisema hakuwa na nia mbaya ya kuondoka na mtoto huyo bali alikuwa akimsaidia kumbebea na alipooulizwa kwa nini aliamua kumuacha na kupanda pikipiki peke yake alishindwa kuongea na alipoangaliwa kwenye mkoba wake alikutwa na kadi ya ujauzito ikionyesha anatarajiwa kujifungua septemba 19 mwaka licha ya kwamba alikuwa hana ujauzito.

Mmoja wa mashusuda wa tukio hilo alisema alimuona mwanamke huyo aliyedaiwa kuiba mtoto kwa siku mbili maeneo ya Nyakato Manispaa ya Musoma kama mgeni karibu na nyumba anayoishi.

Kamanda wa polisi mkoani Mara Ferdnand Mtui amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na Mwanamke anayedaiwa kufanya jaribio la kuiba mtoto anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na baada ya upelelezi hatua zaidi za kisheria zitafuatwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz