Mbunge wa Arusha mjini Godbles amekanusha na kukemea vikali baadhi ya watu wanaomdhalilisha kwenye mitandao ya kijamii kwa kutengeneza na kusambaza picha chafu ambazo zinaonesha udhalilishaji mkubwa kwa mbunge na hata kwa mtu wa kawaida.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake jijini Arusha mbunge Lema amesema picha hizo za aibu zimetengezwa na kusambazwa na mtu ama watu wenye lengo la kumdhalilisha na tayari amekwishaanza hatua ya kuchukua hatua za kufikisha suala hilo kwenye uongozi wa bunge akiwemo Spika Anne Makinda, naibu spika Job Ndugai pamoja na katibu wa bunge.
Amesema ameamua kutoa taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari kwa sababu vitu vikishawekwa kwenye mitandao ya kijamii siyo siri tena hivyo anategemea bunge litaona wajibu na ni jinsi gani heshima ya mbunge imeshushwa na kudhalilisha kwa maksudi bila kujali utu na heshima ya mbunge.
MSIKILIZE HAPA CHINI LEMA AKIZUNGUMZIA ALIVYODHALILISHWA
0 comments:
Post a Comment