Mama Mzazi wa Mwanafunzi anaedaiwa kubakwa, Mary Mkombola akisimulia juu ya tukio la ubakaji lililompata
Mwanae na kusababisha ujauzito mbele ya waandishi wa habari Kulia ni Martha Danie (17) anayesoma shule ya City Sekondari kidato cha tatu aliyefanyiwa kitendo hicho.
Mwanasheria
Mfawidhi Mkazi wa kituo cha msaada wakisheria cha Tanzania Legal Aid
Centre (TALAC), Godwin Ngongi akifafanua jambo kuhusu kitendo cha
ubakaji alichofanyiwa Mwanafunzi wa kidato cha tatu Martha
Nabii Elisha Muliri anayetuhumiwa kwa ubakaji
Na John Banda, Dodoma
NABII Elisha Muliri wa kanisa la Ebeneza mjini hapa ameingia matatani baada ya kudaiwa kumbaka na kumtia mimba mwanafunzi na kukatiza masomo yake huku kutishia kumuua.
Akisimulia
tukio hilo mbele ya waandishi wa habari mwanafunzi huyo Martha Daniel
[17] kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya City ilyopo manispaa
ya Dodoma alisema kabla ya kufanyiwa kitendo hicho alikuwa anaangushwa
na mapepo.
Martha
alisema baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila mafanikio walipata
taarifa za ujio wa nabii huyo mjini humo na wapofika ili kupata msaada
wa kuombewa mapepo hayo yalilipuka na binti akaponywa hata leo na
kuahidiwa mbele ya kanisa kusaidiwa ada na Nabii huyo.
Binti
huyo alisema baada ya kuponywa akaendelea kwenda kusali kanisani hapo
ambapo kutokana na kila mtu anayefika na kufanyiwa maombi huacha
mawasiliono kwenye vikaratasi, na Juni 8 mwaka huu majira akapigiwa simu
na Nabii huyo akipewa maelekezo ya kufika nyuma ya ukumbi wa Paradise
ambapo walikuwa wakifanyia ibada.
Anatanabaisha
kuwa baada ya kuonana Nabii alimwambia aingie kwenye Gari akaingia
akifikili kuna heri akapewa soda aina ya Fanta orange alipokunywa
akapoteza fahamu na alipokuja kuzinduka alijikuta akiwa nyumba za kulala
wageni makole na Nabii akiwa amemlalia kama alivyozali huku akiangalia
mkanda wa Ngono.
‘’Wakati
nataka kupiga kelele alinitishia kwamba ataniua kama nitathubutu
kumwambia mtu yoyote jambo hilo, akanipiga kofi na kuniambia yeye hawezi
kunilipia ada bure kwa sababu mimi siyo ndugu yake lazima lazima alale
na mimi mara 5 kwa hiyo bado mara 4 na kunisisitiza asisikie popote kuwa
alinifanyia hivyo’’, alisema Mwanafunzi huyo
Kwa
upande wake Mama mzazi wa mwanafunzi huyo Mary Mkombora alisema
alimpeleka kuombewa kutokana na kusubuliwa na mapepo tangu akiwa Darasa
la sita na wakakubaliana na Nabii huyo kumlipia ada kwa awamu hivyo
akachukue 50,000 kila mwezi ili kukamilisha 400,000 inayotakiwa shule.
Nilimgundua
yupo tofauti kuanzia mwezi wa saba nilipomuuliza alisema yeyue haelewi
siku moja nikamshuhudia akitapika asubuhi ndipo nilipochapa na kumfukuza
nikapigiwa simu na waliompokea kua mtoto kapewa mimba hiyo na Nabii
kwanini nimemfukuza ndipo nikachoka, alipopimwa alikuwa na mimba.
Alisema
Nabii huyo ambaye alikuwa Mume wa mwimbaji Marufu wa Nyimbo za Injili
marehemu Anjera Chibalonza kwa sasa hajulikani alipo japo mara kadha
wasaidizi wa kanisa hilo ambalo limebadilishwa jina kutoka Shakinah
Pentecostal Church na kuitwa Ebeneza wamekuwa akitaka Suruhu.
‘’sasa
hivi mimi na mtoto wangu tumekuwa tukiishi mashakani baada ya Msaidizi
wake Nabii Monica nimpe Martha akamtoe mimba kwa ataaramu anaowajua
wao, siku ambayo alichukua kadi yenye namba za simu na kufuta meseji
zote mwanangu alizokuwa akiandikiwa na Nabii,’’
Nabii
huyo kwa sasa hajulikani alipo na hata alipotafutwa kwa simu yake ka
mkono 0756 409118 ilikuwa amezimwa na msaidizi wake Nabii Monica
Nyambura raia wa nchini Kenya anakotoea Elisha Muliri alisema yeye
hawezi kuongelea jambo hilo kwakua yeye ni mgeni ameachiwa kanisa hilo
baada ya mwenyeji wake kuwa safarini hivya asubiliwe hatachelewa.
Tukio
hilo limefikishwa katika kituo cha sharia cha Tanzania Legal Centre
[TALAC] na mwanasheria mfawidhi mkazi Dodoma Godwin Ngongi tayali
ameshamuandikia mkuu wa kituo cha polisi kati barua ya kuwataka
kumkamata mtuhumiwa huyo ili afikishwe kwenye vyombo vya sharia na pia
kuepusha mwanfunzi huyo na hatari nyingine.
Jeshi hilo limekiri kuwa na taarifa ya tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi
0 comments:
Post a Comment