VITENDO vya ukatili kwa watoto wenye umri mdogo vimeendelea kushamiri katika jamii, ambapo msichana wa kazi aliyetambulika kwa jina la Anna (13) mkazi wa ngaramtoni wilayani arumeru mkoaani arusha, ameharibika vibaya sehemu zake za siri kutokana na kitendo cha kunajisiwa na kulawitiwa na baba mwenye nyumba wake aliyejulikana kwa jina la Godifrey John(33).
Akizungumza
na mwandishi wetu baada ya kuokolewa na shirika la shaloom center for
street children, linalojihusisha na utetezi wa haki za mtoto, mtoto huyo
anaeleza kuwa, alianza kufanyiwa vitendo vya ukatili tangu April mwaka
huu baada ya kutoka kijijini kwao masumbwe kilichopo wilayani kahama,
mkoa wa shinyanga.
Alisema
kitendo hicho kilikuwa kikimuumiza sana, lakini kadri siku zilivyokuwa
zikisonga alilazimika kuzoea maumivu makali aliyokuwa akiyapata kwani
mwajiri wake alikuwa akishamaliza kumwingilia alikuwa akimtishia kumuua
iwapo angethubutu kutoboa siri hiyo kwa mtu yeyote.
Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano, anaeleza kuwa, bosi wake huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa mazao, alikuwa akimnajisi na kumlawiti kwa kumziba mdomo ili asitoe sauti baada ya kumfungia mke wake chumbani majira ya usiku na mchana hasa kipindi ambacho mkewe alikuwa kwenye hali ya kujifungua.
Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano, anaeleza kuwa, bosi wake huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa mazao, alikuwa akimnajisi na kumlawiti kwa kumziba mdomo ili asitoe sauti baada ya kumfungia mke wake chumbani majira ya usiku na mchana hasa kipindi ambacho mkewe alikuwa kwenye hali ya kujifungua.
Alisema
bosi wake huyo alikuwa akimwacha mkewe kitandani na kumfuata sebuleni
alikokuwa amelala na kuanza kumwingilia kinyume na maumbile huku akiwa
amemziba mdomo ili asitoe kelele wakati akifanyiwa ukatili huo.
''Alikuwa
akiniingilia mara kwa mara, sikumbuki ni mara ngapi, na akianza
kunifanyia mchezo mbaya alikuwa akiniziba mdomo na mkewe alikuwa
akimfungia chumbani kwa komeo na kuna kipindi alikuwa mkali
akinikaripia'' alisema.
Alisema
kuwa, alifika mkoani arusha, mwezi februari mwaka huu, baada ya
kuchukuliwa na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la zawadi samuel ambaye ni
rafiki yake na mtuhumiwa, ambaye alikuwa akihitaji msichana wa kazi
kutokana na mkewe kuwa mjamzito.
"Huyo
zawadi tulikutana nae kwenye basi nikitoka masumbwe kwenda kahama
mjini, akaniambia kuwa anipeleke arusha akanitafutie kazi, nilikubali
tukaondoka kesho yake, ila hadi sasa sina mawasiliano na wazazi wangu na
sina ndugu yeyote hapa arusha,'' alisema anna.
Aliongeza
kuwa katika kipindi cha miezi 8 alichofanya kazi kwa mtuhumiwa huyo,
hakuwahi kulipwa mshahara ambao walikubaliana shilingi 20,000 kwa mwezi,
ila aliwahi kumpa shilingi 10,000 na kumnunulia sketi mbili tu.
Alieleza
kuwa mbali na kumfanyia unyama, alikuwa akimtesa kwa kumfanyisha kazi
nyingi ikiwemo kumlazimisha kusomba maji umbali mrefu bila kupumzika,
huku akishindwa kumsomesha kama alivyoahidi kufanya hivyo hapo awali.
Kwa
upande wa mwakilishi wa shirika la shaloom center, Enezael Joseph
alisema kuwa wamefanikiwa kumwokoa mtoto huyo katika mazingira magumu
baada ya kupata taarifa kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji
kinyume cha sheria.
Alisema
kuwa shirika hilo lilipata taarifa kutoka kwa majirani wa mtuhumiwa
ambao walichoshwa na vitendo vya manyanyaso anavyovipata mtoto huyo na
kuamua kumfuata mtoto huyo na kuzungumza naye ndipo alieleza mambo
mazito ya kulawitiwa na kunajisiwa naa mtuhumiwa kila kukicha.
Joseph
anasema kuwa baada ya taarifa hizo walitoa taarifa kituo cha polisi
ngaramtoni na kupewa hati ya matibabu (PF3) ambapo msichana huyo baada
ya kupimwa katika hospitali ya seliani ya jijini arusha, aligundulika
kuharibiwa vibaya sehemu zake zote za siri.
Alisema
baada ya kupata majibu ya dakitari walirejea na kuwakabidhi polisi
ambapo walifungua hati ya mashtaka ya kulawiti yenye kumbukumbu namba
NGT/RB/1113/2013 ambapo mtuhumiwa alikamatwa na taratibu za kumfikisha
mahakamani zinaaendelea.
Hata
hivyo mtuhumiwa wakati akitiwa mbaroni alisikika akidai kwamba
anachofahamu kwa msichana huyo ni kwamba anamdai fedha zake za mshahara
ila hayo madai mengine si kweli kwani amepandikizwa ili kumdhalilisha.
0 comments:
Post a Comment