Balozi Isaac Abraham Sepetu alizaliwa
October 15, 1943, ni mzaliwa wa Tabora ila alikulia Zanzibar na alikuwa
ni mkaazi wa Zanzibar mpaka mauti yanamfika
Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu
alipata elimu yake ya msingi na sekondari katika shule ya St.joseph’s
kwa sasa inaitwa Tumekuja huko Zanzibar mnamo mwaka 1952 hadi 1963,
vilevile aliweza kujiunga na chuo kikuu huko Berlin nchini Ujerumani
mwaka 1964 hadi 1970 alisomea Shahada ya Uchumi,
Marehemu alikuwa anauwezo wa kuongea lugha tatu (3) kwa ufasaha ambazo ni ;- kiswahili, kingereza na kijerumani.
KAZI
Alianza kufanya kazi katika Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 1971 hadi 1972 kama Mkuu wa Bizanje Msaidizi
na pia alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ikulu. Baada ya hapo mwaka
1972 hadi 1977 alikuwa Naibu Waziri Mambo ya Nje katika serikali ya
Muungano Zanzibar, mnamo mwaka 1977 hadi 1979 Marehemu Balozi Isaac
Abraham Sepetu alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji, Ilipofika mwaka
1979 hadi 1982 alikuwa Waziri wa Utalii na Maliasili .
Marehemu Balozi Sepetu mwaka 1982
hadi 1989 alipewa nafasi ya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Moscow
na mwaka 1989 hadi 1990 alikuwa Balozi wa nchi ya Zaire, Kinshasa
Katika Serikali ya Mapinduzi
Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Waziri
wa Nchi, Mipango pia alikuwa Mshauri wa Rais, Ushirikiano wa Kimataifa
na pia alikuwa Katibu , Kamati ya Pamoja(IPC) CCM/CUF, Zanzibar Mwaka
2001 hadi 2005 alikuwa mbunge wa bunge la Afrika ya Mashariki
Uzoefu wa Kisiasa
Mwaka 1977 hadi 2005 alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi
0 comments:
Post a Comment