Watu
wawili wanaotuhumiwa kuwa ni wezi a.k.a Wapigaji/Matapeli wamekamatwa
usiku huu kwenye hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.
Watu
hao ambao wamekamatwa ni Bw. Takula Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na
Bw. Juma Hamis ambaye ni mkazi wa Tabata wakiwa na nyaraka tofauti
ikiwemo kitambulisho kinachotaja kuwa ni cha Idara ya Usalama wa Taifa,
kadi za benki pamoja na simu zaidi ya kumi,wakiwa katika harakati za
kumtapeli mwanadada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni
Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara cha CBE,Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar
es Salaa .
Akisimulia
tukio dada huyo ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya
wiki iliyopita alisema kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa
katika fukwe wakipunga upepo ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na
baadae aliwawekea madawa ya kulevya na kuondoka na dada huyo kwenda
kumtupa baharini.
Kava ya nje ya Kitambulisho hicho kinaonekana namna hii.
Watuhumiwa hao wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi.
Kitambulisho hicho kinavyoonekana kwa nyuma.
Mtuhumiwa
wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis huku akiwa na
Kitambulisho cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la
Kenedy Magige.
Mtuhumiwa
mwenza wa Tukio hilo la Wizi,aliejitambulisha kwa jina la Takula
Manyenga mwenye umri wa Miaka 28,akidhibitiwa kwa kufungwa kamba mara
baada ya kukamatwa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es
Salaam.
Watuhumiwa wote wawili wakipakiwa ndani ya Gari la Polisi kutoka katika Kituo cha Kawe,Jijini Dar es Salaam.
Askari Polisi wakiwa eneo la tukuo kuhakikisha Usalama unapatikana eneo hilo.
Askari
Polisi wakiwa na Watuhumiwa hao wakati wakiendelea na Ukaguzi ndani ya
Gari hilo aina ya Toyota Prado lenye nambari za Usajili T 445 BCY.
Askari
Polisi wakiendelea na Ukaguzi ndani ya Gari hilo,ambapo ndani ya Gari
hilo kulikutwa na Simu zaidi ya kumi ambazo zilichukuliwa na Polisi hao.
Gari walilokuwa wakilitumia Watuhumiwa hao.
Ulinzi mkali kwa watuhumiwa hao.
Msafara wa kuelekea kituoni.