Victoria Mukama (10) baada ya matibabu
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba
mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama mkazi wa Isengo Airport
Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga
sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo
Lungu.
Kwa
mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule
ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea
majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi
huyo
akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.
Alisema mzazi huyo baada ya kufika
walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu
mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya
kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.
Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza
kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo
alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi
yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu
wamwadhibu.
Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na
kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule
alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa
taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu
(PF3) kwa ajili ya matibabu.
Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo
alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka
Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza
sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na
kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya
kwenda kazini kwake anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za
shule na kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.
Alisema alishikwa na butwaa hadi
kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na
mumewe kwamba aende shule kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa
kiasi cha kumjeruhi mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.
Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake
baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha
dharula, Victoria Mukama (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika
Shule ya Msingi Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa
akianza kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.
Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka
nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi
Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya
kuwatishia wanataka kumuokoa.
Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi
linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya
kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha
Polisi Mbeya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa
Pambogo Esia Edward ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo
alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa
macho hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo
vinakomeshwa ndani ya jamii.
Aliongeza kuwa hajawahi kusikia
mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na ukatili wa namna hiyo na kuongeza
kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao
mbali mbali vinavyoitishwa pamoja na kuchangia mada.
Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai
kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye
anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya
kuandika makosa anayotendewa na mkewe.
Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa
nae watoto watatu lakini mkewe huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya
unyanyasaji imezidi kutoka kwa Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu
wa Mosoma Mkoani Mara ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado
zinafanyika.
-MBEYA YETU
|
0 comments:
Post a Comment