Link Mbaga baada ya kula kichapo cha nguvu kutoka kwa wananchi wenye hasira kali |
MKAZI mmoja wa Sinza Lion jijini Dar, Link Mbaga (25) Jumanne iliyopita alinaswa maeneo ya Sinza Afrikasana na kuchezea kichapo kutoka kwa watu wenye hasira akidaiwa kutaka kuiba vifaa vya kwenye gari aina ya Toyota Harrier, Ijumaa limeinyaka.
Mbaga akisulubiwa na wananchi.
|
Gari aina ya Toyota Harrier walilotaka kuiba power window Mbaga na wenzake. |
“Kabla ya kumalizia zoezi lao mlinzi wa hospitali hiyo aitwaye Jonas Mwakajinga aliwasikia ndipo alipofika na kuwakurupusha,” kimesema chanzo hicho.
Wananchi wakiwa wameandaa tairi tayari kumtia kiberiti Mbaga kabla ya polisi kufika eneo la tukio na kumnusuru. |
Wakati mlinzi akipambana na Mbaga wananchi wenye hasira walifika eneo la tukio na walipopata maelezo walianza kumpa kichapo cha kufa mtu mtuhumiwa huyo wakisema itakuwa fundisho kwa wengine.
Kipondo kikiwa kimepamba moto kwa Mbaga. |
“Mimi kazi yangu ni data manager niko maeneo ya Mlimani City, naishi Sinza Lion kwa Massawe,” alisema kijana huyo.
Mbaga akiwa hoi baada ya kichapo. |
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
“Nilikuwa nakunywa Pombe na Leonard pale Mlimani City, jamani naomba
mnionee huruma, wale jamaa walinipa lifti tu,walikuwa wako wanne ila
nawafahamu,” alisema Mbaga.
Polisi wakijaribu kuchukua maelezo ya mtuhumiwa baada ya kuwasili eneo la tukio.
Polisi wakimbeba Mbaga kumpeleka kwenye difenda. |
Kutokana na hali mbaya ya mtuhumiwa huyo, askari hao walilazimika kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala ili aweze kupata matibabu.
Mbaga akiingizwa kwenye difenda. |
Safari ya kuelekea Mwananyamala ikaanza. |
1 comments:
awataje sasa
Post a Comment