Leo nitazungumzia suala la penzi kuchuja. Ipo hali ya kujisahau baada ya wapenzi kuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, haieleweki kama ni tabia ya mtu ama ni uhalisia wa mambo kwasababu ukweli ulio wazi ni kwamba, mwanzo wa uhusiano wengi hujitahidi kufanya mambo mengi ya kuwafurahisha wapenzi wetu lakini kadiri siku zinavyosogea, penzi huanza kuchuja.
Kama huamini katika hili, rudisha nyuma kumbukumbu zako kipindi kile
ambacho ndio jamaa kaamua kukueleza wazi kwamba anakupenda halafu
angalia na sasa hivi, utabaini kwamba kuna tofauti kubwa sana.
Huenda mlikuwa na desturi ya kununuliana zawadi kama maua, kadi,
chokoleti tabia hiyo huenda ikawa imeyeyuka, hakuna kati yenu
atakayekumbuka kitu hicho, ni wachache sana ambao wanakwenda na wakati
ndiyo huendelea kuzingatia hayo.
Kuna wale ambao walikuwa na tabia ya kukutana kila mara kimapenzi ambapo
kila mmoja alitaka kumuonesha mwenzie jinsi alivyo fundi wa 'kuyarudi'
ndani ya uwanja wa mapenzi lakini yale manjonjo huadimika kabisa.
Kawaida yenu ilikuwa kubadilisha hoteli kwa ajili ya chakula cha jioni
lakini tabia hiyo hutoweka, labda kila wiki ilikuwa lazima muende 'out'
mara tatu katika kumbi tofauti za starehe na kufurahia mapenzi yenu,
hali hiyo itabaki historia tu.
Hivi hujawahi kusikia mtu anasema "Enzi zile naanza uhusiano na mpenzi
wangu mapenzi yalikuwa moto moto, kila wiki ilikuwa lazima twende beach
lakini, siku hizi nikigusia tu kwenda huko ni ugomvi."
Maneno kama haya huwa yananiuma sana hasa ninapogundua kwamba walio
wengi wanakuwa na nguvu ya soda pale wanapoingia katika uhusiano lakini
baada ya muda mambo hubadilika kabisa.
Sijajua ni kwasababu gani lakini kwa utafiti mdogo ambao nilioufanya kwa
baadhi ya wanaume ni kwamba, wao wanapofanikiwa ‘kuona ndani tu’
hujenga kiburi fulani kwa wasichana wao huku wakiamini kwamba, hata wawe
tofauti vipi hawawezi kuachwa!
Labda nijaribu kushauri kitu katika hili kwamba, kama uko kwenye
uhusiano wa kimapenzi ama uko ndani ya ndoa, unatakiwa kufanya kila
linalowezekana kulifanya penzi lenu lisichuje.
Wewe ndio unaweza kulifanya likaendelea kuonekana kuwa jipya kila siku
ama kulifanya likachuja mithili ya nguo inayochuja rangi iliyotumbukiza
katika ndoo ya maji ya moto.
Hatukatai kwamba, kuna mabadiliko ya kimaslahi, pengine mtu na mpenzi
wake wameketi na kuona wanatumia pesa nyingi viwanja, kwahiyo wanaamua
kupunguza au kuacha ili kujenga maisha bora ya baadae, si unajua tena
mnapokuwa na malengo ya kimaisha zaidi?
Lakini ukweli unabaki palepale kwamba, penzi la dhati haliwezi kuchuja
hata siku moja. Tujue wapo ambao wameishi miaka zaidi ya hamsini lakini
penzi lao bado ni moto licha ya kuwepo kwa mabadiliko madogo ambayo
hayakwepeki kutokana na umri.
Yapo mabadiliko mengi, lakini zaidi tujirekebishe, tukumbuke kwamba
baadhi ya vitu tulivyokuwa navyo huko nyuma ndivyo viliwavutia wepenzi
wetu na kukubali kuwa nasi kwa hiyo tukiacha tunakuwa tunawakatili.
0 comments:
Post a Comment