DOGO JANJA AFUKUZWA RASMI MTANASHATI ENTERTINMENT...TABIA MBAYA NDIO CHANZO

Msanii mdogo aliyewahi kutamba katika tasnia ya muziki wa bongo fleva Dogo Janja amefukuzwa rasmi Mtanashati Entertinment, Taarifa zilizofikia dawati letu la habari zinasema Dogo Janja amefukuzwa na Ostazi Juma Na Musoma baada ya kushindwana kitabia, Hapo awali Dogo Janja aliwahi kuwa mwanakundi la Tip Top Connection lililo chini ya uongozi wa Madee hata hivyo alifukuzwa na kurudi kwao Arusha ambapo Ustazi Juma Na Musoma alimfuata na na kumuweka kundini huku akimuhudumia katika kila jambo ambalo alitakiwa kupata kama
mtoto na mwanamuziki pia. Lakini Leo imefika tamati ya Ostazi Juma na kuamua kumuacha Dogo Janja aende zake.



Vile vile kutoka katika kundi hilo la Mtanashati Kuna nyimbo mpya ya msanii PNC inayokuja hivi karibuni, ni Bonge moja la track linakwenda kwa jina la HABARI YA MJINI, nyimbo hii itayoachiwa hvi karibuni itakuja pamoja na video kali. Jiandae kwa nyimbo kali kutoka kwa PNC

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz