Taarifa ambazo
tumezipata kutoka ndani ya kikao cha Baraza la uongozi kanda
ya Kaskazini, kilichofanyika katika Hotel ya Corridor Spring leo usiku, zimedai uamuzi wa kusimamishwa Mwigamba umefikiwa na
Kikao hicho baada ya kuwasilishwa kwa vielelezo kadhaa vya Mwigamba
na yeye kukiri kuwa ni vyake
huku vingine vikimuonyesha kuwa ndiye mmiliki wa Akaunti ya Jina la
‘Maskini Mkulima’ ambalo limekuwa likitumika kukichafua chama kwenye
mitandao ya kijamii.
Hakuna kiongozi ambaye
amekuwa tayari kuzungumzia suala hili kiofisi, lakini taarifa za uhakika ambazo tumezipata kutokana na maamuzi ya kikao hicho
zimebainisha kuwapo kwa maamuzi hayo pasipo shaka.
“Kikao hicho
kimemsimamisha Uongozi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili,
hivyo kuanzia sasa mwigamba siyo kiongozi, nadhani tamko litatolewa
baadaye,” alieleza mmoja wa wajumbe wa kikao hicho
kilichofanyika Arusha na kuongeza kuwa katika Kompyuta yake baadhi ya
maandiko ambayo yamekuwa yakikikashfu chama yamekutwa ikiwa ni pamoja IP
address ya Jina na Maskini Mkulima ambalo limekuwa likituma post ndani
ya Jamiiforums kukuta zinafanana.
Jina la ‘Maskini Mkulima’ lilijiunga na mtandao wa jamiiforums
mnamo Desemba 27, 2011 na mpaka jana inaonyesha alikuwa ametuma zaidi
ya Post 27 ikiwamo hii iliyokuwa na kicha cha habari: Wito kwa wana
CHADEMA wote.
Makala
hiyo ambayo ndiyo imefanikisha kumbaini ilitumwa Jamiiforums Oktoba 19
Mwaka huu chini ya kichwa cha habari cha ‘Wito kwa wana CHADEMA wote!’, inaeleza haya;
Kufuatia malumbano
yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo
tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote
nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.
Kihistoria, CHADEMA
kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili.
Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa
raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa
matukio.
Naandika nikiwa mwana
CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na
kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana
chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.
Nimekuwa mwanachama
wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa
nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika.
Nadriki kusema kwamba
kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM
inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima
matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto
utakuwa ndo mwisho wake.
CHADEMA iliyopiga
kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya
vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM
kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC)
kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha
zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake
nini?
Kama chama
kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri
kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka
zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?
Napenda kabla
sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao
kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala
yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu.
Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa
wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote
tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya
kila mwanachama.
Ni kwa msingi huo
waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote
katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza
kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza
kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya hapo hawezi kugombea
tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili.
Ili
kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi
kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali
wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.
Napenda pia
kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia
chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi
kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani.
Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49.
Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49.
Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake
CHADEMA imebeba agenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi,
utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk.
Lakini kuna matatizo
yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza
kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake
umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye
hakuna CHADEMA.
Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti
mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama
hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga
chini uchaguzi ujao.
Leo nitaainisha mambo
machache tu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema
muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia
wanatakiwa kuwasilisha ripoti za fedha wakajikuta wanapambana na
mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau
kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu
mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata
fursa:
1. Wakati tukifanya
mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia
kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya
miaka mitano mitano.
Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi
uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi
leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa
maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa.
Hiki
kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu
wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi
kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari
zisizomithirika kwa chama.
Ni muhimu wanachadema
mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho
kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto
kupigania uenyekiti.
Kama kingekuwepo leo Mbowe alikuwa anakatazwa na
katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na
Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi.
Ni dhahiri Mbowe
aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila
mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John
Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe,
bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.
2. Matumizi ya fedha za chama:
Hakuna mtu anayejua
hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu
yaani Mwenyekiti Taifa, katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha.
Maamuzi ya
vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010
vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali
zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo
si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha.
Watu watatu ndo
wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza
kuu cha mwezi January kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka
serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine
kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa
ipasavyo.
Nyinyi viongozi wa
kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna
michango ya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani
zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje.
Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye
fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo
nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao
kwenye masuala ya fedha ni questionable.
3. Taarifa za fedha
Tokea baada ya
uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na
kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama.
Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu niliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao.
Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.
Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu niliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao.
Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.
4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
Wakuu waliopo hawana
hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya
‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana
kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya
matukio.
Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama
litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi,
na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha
imebaki ndoto ya mchana.
Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata
uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki
lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.
5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
Chama chetu kinayo
kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii
haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda
kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa.
Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya
magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa
ofisini kwa katibu mkuu, hawana.
Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu
bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya
kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye
aliyenunua magari na pikipiki zote za M4C.
Hivi tunavyoongea
kuna shilingi milioni 80 ambazo mwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza
kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi
kuonekana.
Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye
ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya
katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake ya tenda. Huu si
ufisadi ni nini?
6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama
Hakuna kikao chochote
cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba
sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama
kinanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama
bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti
Taifa na Katibu Mkuu wake tu.
Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge
kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala
ama pinzani.
Pili namshauri CAG
unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala,
na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini
kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo.
Hapo nenda
mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko
zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee.
Pia kuna mkakati
unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi
wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa mikubwa kama Mwanza, Arusha,
Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe matamko kumpinga Zitto.
Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la kamati ya bunge na
kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama.
Hata kama jambo
lenyewe lingekuwa limeagizwa na Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya
kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi wetu wakuu watoe ripoti kuthibitisha
uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli pia kwamba kwenye ripoti
wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika.
Kama ni matamko
toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na hapo ndipo
mtakapo jua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo na
ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.
Nitaendelea kuwadondolea ili muone kwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.
Ahsanteni kwakunisoma!
Masikini Mkulima
Masikini Mkulima