Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
MEMBA wa tasnia ya filamu za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’
amefikishwa kizimbani kwa kosa la kumtusi babu wa miaka 83 kwa kumwambia
kuwa ana Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi)Mbali na kosa hilo, Jini Kabula ambaye alipandishwa katika Mahakama
ya Mwanzo ya Kinondoni jijini Dar, anadaiwa kumtolea matusi ya nguoni
babu huyo anayetambulika kwa jina la Emmanuel Macelemona.
Inadaiwa kuwa mwigizaji huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Julai 24, mwaka huu na kusomewa mashtaka kwa kesi namba 649/13 mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira.
Kwa mujibu wa chanzo chetu mahakamani hapo, siku hiyo Jini Kabula alifika akiwa amevaa kininja ili watu wamsimtambue.
“Kweli alipofika hapa hakuna aliyemjua, akaendelea na kesi yake hiyo ya kutukana na kumnyanyapaa mzee wa watu,” kilisema chanzo chetu mahakamani hapo.
Aidha, chanzo hicho kilisema Alhamisi iliyopita ilikuwa hukumu ya kesi hiyo lakini Jini Kabula pamoja na mdhamini wake hawakutokea mahakamani hapo.
Baada ya kupata taarifa hizo, tuliongea na mwigizaji huyo kwa njia ya simu na kumuuliza kuhusu kesi inayomkabili lakini alikataa na kusema hajawahi kufika mahakamani tangu mwaka huu uanze.
“Mi sina kesi Mahakama ya Kinondoni na tangu mwaka huu uanze sijakanyaga hata mara moja ila nakumbuka kuna kipindi nilikuwa namsindikiza mdogo wangu aliyekuwa na mambo yake,” alijibu Jini Kabula.

0 comments:
Post a Comment