Mkazi
wa Kawe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina
la Musa Senkando anatafutwa na polisi kwa mahojiano baada ya kutoweka
akisadikika kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Yusta Mkali.
Mauaji
hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo(jana)habari za kuaminika za mauaji
hayo kutendeka zilizibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni,
Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kwa
uchunguzi wa awali mauaji hayo yanasadikika kutokea usiku wa kuamkia
leo.
“Yusta
ameuwawa na kitu chenye ncha kali kilichomchoma kwenye koromeo na
inasadikika mume huyo ameshatoweka na jeshi la polisi linamtafuta kwa
uchunguzi zaidi kwani yeye ndiye aliekuwa mtu wa mwisho kuwa nae ndani,”
alisema.
Wambura alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Naye
Mtoto wa dada yake marehemu ambaye alikuwa anaishi naye, Joshua
Zebedayo alisema yeye ameshtukizwa na mauaji hayo pale alipo amka
asubuhi kuelekea kufanya usafi chumbani mwa mama yake mdogo kwani yeye
huwa analala chumba kingine na ndipo alipoukuta mwili wa marehemu ukiwa
na majeraha pamoja na damu.
“Ilikuwa
majira ya saa mbili asubuhi nilipoamka kufanya usafi chumbani kwa mama
kama ilivyokawaida yangu mama na baba waendapo kazini, ila cha
kushangaza nilimkuta mama bado amelala wakati alitakiwa kuwepo kazini.
Nilimwita mama bila mafanikio nikafunua shuka alilojifunika na kumkuta
amekwisha fariki dunia,” alisema kijana huyo huku akibubujikwa na
machozi.
Marehemu Yusta wakati wa uhai wake,alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya umma Frontline Porter Novelli(PR COMPANY)
Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake. |
Wakazi wa Kawe wakiwa na nyuso za huzuni wakati mwili wa marehemu ukitolewa ndani kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. |
Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukitolewa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. |
0 comments:
Post a Comment