Manaiki Sanga "the don "
Libert Msuya kulia pamoja na picha nyingine tofauti.
Mfanyabiashara
maarufu na msanii nyota wa bongo muvi ambae ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafua
aliyefahamika kwa jina la Libart Msuya katika ya wiki hii alionja joto ya jiwe
baada ya kuhenyeshwa masaa kadhaa kwa kupekuliwa alipokuwa anareja toka nchini
Uingereza huku msanii mwenzake Manaiki Sanga akihangaika kumnusuru.
Habari za
uhakika zilizonaswa ambayo ilikuwepo kwenye viwanja hivyo kwa ajili
ya kumpokea mzanii Azonto ambapo Libart alisafiri ndege moja na Azonto
wakitokea Uingereza ilishuhudia jambajamba hiyo aliyokuwa akipewa Libert kwenye
sehemu ya kutokea wageni wanaokuwa wanawasili.
Libert Msuya
ambae ana uaraia wa Ungereza licha ya kwamba ni mtanzani siku za hivi karibuni
alikuwa nchini huko ndio familia yake ilipo na siku hiyo ya tukio alikuwa
anarejea Tanzani huku akiwa na mabegi
kibao na baada ya kufika Air Port ya Dar mabegi hayo alifanyiwa uchunguzi
mkubwa kiasi cha kusababisha askari wote kumzunguka.
Hata hivyo
hali hiyo iliyodumu kwa dakika 40 ilimlazimu rafiki wa karibu na mtoto huyo
Manaiki Sanga “The Don” kuanza kuchanganyikiwa akizani labda huenda ni kweli
rafiki yake huyo alikuwa na mzigo.
Aidha baada
ya kuachiwa huru Libert alitoka nje huku akipokelewa na Manaiki, hata hivyo
mwandishi wetu alifanikiwa kuongea na Libert ambae alisema “ Ni utaratibu ambao
upo kila nchi wa kusachiwa hivyo mimi sikuona tatizo pele na wala mimi
sijihusishi na biashara yoyote haramu” Alisema Libert
Hata hivyo
nae msanii Manaiki Sanga” The Done” aliiambia blog hii kuwa biashara ya madawa
sio rahisi kama inafanywa na watu wenye mioyo migumu huku wakiwa wamekula viapo
kwamba lolote litakalotokea poa na sio kazi rahisi ni kama sanaa wanayoifanya
wasanii wote.
0 comments:
Post a Comment