skip to main |
skip to sidebar
Ukifuatilia ratiba za
maisha ya anasa ya kila siku ya mastaa wa Kibongo, lazima utajiuliza kwa
nini wasiuze au kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’?
Uchunguzi uliopewa sapoti
na baadhi ya mastaa hao, ulibaini kwamba suala la kupenda kujirusha
kuliko kazi ndiyo chanzo cha kufanywa ‘punda’ wa kusafirisha unga na
matokeo yake kunaswa na kuingia kwenye matatizo makubwa.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa kuna baadhi
ya mastaa hao, ratiba zao za kujirusha na kula bata ndefu zimewabana
kiasi cha kushindwa kuendeleza vipaji vyao katika sanaa.
Ratiba za baadhi ya mastaa hao za kujirusha ni kama ifuatavyo;
JUMATANO
Ilibainika kuwa Jumatano, baadhi ya
mastaa hao hupenda kwenda kujirusha kwenye kumbi za starehe hasa katika
Klabu ya Bilicanas, Posta ambako mara nyingi kunakuwa na bendi
inayomwaga burudani huku wakishushia na pombe.
Ilibainika kuwa mastaa hao huondoka
kwenye kumbi hizo za starehe karibia kunakucha (majogoo) huku wakiwa
‘tilalila’ na kwenda kulala.
ALHAMISI
Data zilizopatika kwa kumsoma msanii
mmoja baada ya mwingine zilibaini kwamba, kwa kuwa huchelewa kulala
Jumatano huku wakiwa na uchovu, Alhamisi huamka saa 10:00 jioni kisha
kuchati kidogo na marafiki kabla ya usiku kwenda kujirusha hasa New
Maisha Club kunakokuwa na burudani ya bendi.
Ilibainika kwamba wakiwa humo hujiachia kwa ‘masebene’ na kugonga pombe kama ilivyokuwa jana yake hadi majogoo.
IJUMAA
Uchunguzi ulibaini kuwa siku ya Ijumaa,
baadhi ya mastaa hao huamka tena saa 10:00 jioni na kinachoonekana ni
kati ya siku ‘bize’ kwa mambo ya starehe hivyo wanakuwa na mialiko
mingi.
Ilibainika kuwa baadhi yao huhudhuria
mialiko ya sherehe za harusi, send-off, kitchen party, birthday na
nyinginezo kabla ya baadaye kumalizia kwa kwenda kwenye ‘live’ bendi.
Mara nyingi hupenda kuhudhuria kwenye
shoo kama hizo katika Kumbi za Thai Village, Masaki, Nyumbani Lounge,
Ada Estate, Kinondoni au Club 24, Mikocheni ambako huko nako hukesha
hadi majogoo.
JUMAMOSI
Uchunguzi wetu ulibaini kwamba Jumamosi,
baadhi ya mastaa hao huamka saa 10:00 jioni kama kawa kisha kunyoosha
miguu hadi baa ambapo giza likiingia huzama tena kwenye burudani ya
bendi.
Wengi hupatikana katika kumbi
zinazoungurumisha muziki wa bendi za dansi. Huko nako huwa wanakula bata
ndefu hadi majogoo kisha kurejea nyumbani kulala.
JUMAPILI
Kama kawaida, baadhi ya mastaa hao
huamka saa 10:00 jioni kisha kwenda kujipumzisha ufukweni hasa Coco na
kuendelea kujirusha. Usiku mnene ‘hujimuvuzisha’ kwenye klabu za starehe
ambapo ama msanii wa Bongo Fleva anazindua wimbo au kunakuwa na shoo ya
kawaida ya muziki.
Kumbi za starehe zinazokuwa ‘bize’ na
mastaa huku kukiwa na shoo usiku wa Jumapili ni pamoja na Bilicanas na
New Maisha Club ambako huko nako huondoka majogoo kwenda kulala.
JUMATATU
Ilifahamika kuwa siku ya Jumatatu baadhi
ya mastaa hao huamka saa 7:00 mchana kisha kwenda saluni na baadaye
kufanya ‘window shopping’ katika maduka ya nguo, supermarket na sehemu
nyingine.
Baada ya hapo muda wa jioni, baadhi ya
mastaa hao hupendelea kwenda kuogelea (swimming) kisha kuibuka Coco
Beach kupata mihogo ya kuchoma, mishikaki, ‘shisha’, pombe na starehe
nyingine za kiutu uzima.
JUMANNE
Mara nyingi uchunguzi wetu ulibaini kuwa
siku ya Jumanne hutumiwa na wasanii hao kupumzika kutokana na uchovu wa
wiki nzima kabla ya ratiba kujirudiana tena kuanzia Jumatano.
WENYEWE WANASEMAJE?
BABY MADAHA
“Mimi naweza kujiachia kila siku lakini
mara nyingi natoka siku tano na ratiba zinaendelea kama kawa maana huwa
nalala mchana na nikitoka narudi saa 9:00 usiku.”
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
“Siku hizi natoka mara mojamoja siyo kama zamani lakini nikiwa na kampani huwa narudi kulala saa 10:00 usiku.”
TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
“Mimi huwa natoka kwenye ishu maalum tu.”
JACQUELINE PATRIC
“Naweza nisitoke wiki nzima lakini nikijisikia pia naweza kutoka wiki nzima na mambo mengine yanaendelea.”
WATOTO WA MBWA (TIKO, MARY & THEKLA)
“Siku hizi huwa tunatoka siku maalum, siyo kama zamani.”
YOBNESH YUSUF ‘BATULI’
“Inategemea, kama nimealikwa sehemu narudi saa 10:00 usiku au asubuhi maana kazi zetu siyo za kila siku.”
LULU MATHIAS ‘AUNTY LULU’
“Huwa natoka siku ya Ijumaa narudi saa 8:00 usiku naamka 4:00 asubuhi. Pia natoka Jumapili kwa sababu Jumatatu nakuwa off.”
KWA NINI WASIUZE UNGA?
Uchambuzi wa kina ulibaini kuwa mbali na
starehe hizo, pia kuna masuala ya mapenzi ambayo nayo huwa ni gharama
na pia hutumia muda wao mwingi.
Ilibumburuka kuwa kwa staili hiyo ya
maisha ya anasa huku baadhi wakisahau kwenda studio kurekodi na mazoezi
ya shoo (kwa wanamuziki) na kutoonekana lokesheni wakishuti filamu.
Ilifahamika kwamba kwa ratiba hizo,
anapotokea kigogo (mfanyabiashara wa madawa ya kulevya) na ‘kumsomesha’
msanii kuwa kuna dili la unga lazima akubali kuwa punda ili apate fedha
za harakaharaka za kutanulia asiachwe na watoto wa mjini.
Listi inazidi kuongezeka kila kukicha ya
mastaa mbalimbali ambao wanadaiwa kunaswa na unga wakiwemo Agness
Gelard ‘Masogange’ na shosti yake, Mellisa Edward, Sandra Khan ‘Binti
Kiziwi’, Saadah Ally, Aisha Bui, Mkwanda na Mbwana Matumla, Joseph
Kaniki na wengineo.
0 comments:
Post a Comment