Raia wa nchini Canada ambaye
ni mfanyakazi wa kampuni ya African Barrick Gold Bulyanhulu aliyefahamika kwa
jina la Andre Lapierre (50) amefikishwa mahakama ya mwanzo Lunguya
wilayani kahama mkoani shinyanga kwa kosa la kutelekeza mtoto kinyume cha
kifungu namba 166 cha sura ya 16 aliyezaa na Bi Elizabeth John.
Akisoma makosa hayo hakimu wa mahakama ya mwanzo Lunguya Derck Masaga ameiambia mahakani hiyo kuwa katika shitaka hilo Andre Lapierre mwaka jana alimpatia hujauzito Elizabeth john(21) mkazi wa kakola.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa Raia huyo wa Canada alimpatia ujauzito Elizabeth na kupata mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka moja na nusu sasa na kumuacha bila matumizi.
Kwa upande wake mtuhumiwa huyo Andre Lapieree alipoulizwa mahakamani hapo juu ya suala hilo la kutelekeza mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Mariam Andre amesema kuwa siyo kweli kuwa yeye amemtelekeza mtoto huyo.
Akiezea zaidi mahakamani hapo Lapierre amesema yeye hana mashaka na mototo huyo hivyo anaiomba naomba mahakama hiyo , wakapimwe vipimo vya ( DNA) ili ukweli ujulikane.
BI ELIZABETH JOHN AMBAYE AMEZAA NA MZUNGU ANDRE
LAPIERRE (50) MFANYAKAZI WA MGODI WA BULHYAHULU AMBAO UNAMILIKIWA NA AFRICAN
BARRICK GOLD MINE LTD AKIWA KATIKA MAHAKAMA YA MWANZO LUGUYA
WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA ALIPOFUNGUA KESI HIYO YA KUTELEKEZWA KWA MTOTO.
Hata hiyo mahakama ilisikiliza hoja hiyo na kutaka kupata upande wa mlalamikaji juu ya suala hilo la kukubali kwenda kwenye vipimo vya( DNA) katika hospital ya serikali na mkemia mkuu wa serikali na tasisi za serikali si mahali pengine.
Mahakama ilimuliza Elizabeth kama yupo tayari kwa mtoto wake kupimwa vipimo hivyo naye alisema yuko tayari kwa kuwa hana wasiwasi kuwa mtoto huyo baba yake ni Endrue.
Mshitakiwa Endrue Lapieree
yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili na kutoa
shilingi milioni moja.
kesi hiyo ya jinai yenye
namba namba 245/2013, imeharishwa hadi tarehe 4 mwezi wa kumi mwaka huu 2013.
0 comments:
Post a Comment