BABY MADAHA AONYWA KUHUSU UNGA NA POMBE

MWANADADA anayefanya vizuri katika anga la Muziki Bongo,  Baby Joseph Madaha,  ametahadharishwa na baadhi ya wadau wa burudani hapa nchini  kutoshawishika na matumizi ya  madawa ya kulevya pamoja na unywaji wa pombe kupindukia kufuatia taarifa za hivi karibuni kuweka wazi mpango wake wa kupiga kambi nchini Kenya.

Madaha ambaye ‘amekwaa dili’ la kufanya  kazi chini ya Kampuni ya Candy n’ Candy Records inayoongozwa na Joe Kairuki na iliyoko jijini Nairobi,   ameshauriwa hivyo kufuatia madai ya msanii mwenzake Rehema Chalamila kutopea zaidi kwenye matumizi ya madawa hayo baada ya kuhamia nchini humo kwa mgongo wa kazi ya muziki.
“Hatuna tatizo na  Madaha kwenda kufanya muziki Kenya, tunachotahadharisha ni kuwa  makini ili asije akaharibika kama Ray C ambaye alipokuwa Kenya ndiko alikozidisha utumiaji unga na unywaji wa pombe kupitiliza,  tunajua Madaha ni mfuasi mzuri wa pombe, atulie na afanye kazi zake ,” alisema mdau mmoja wa burudani aliyejitambulisha kwa jina moja la Marcus.
Ijumaa lilimtafuta Madaha kuzungumzia maoni hayo ambapo alisema: “Nakwenda kufanya muziki wa kimataifa, nitapunguza starehe zisizo na ulazima na kuhusu madawa ya kulevya hayana nafasi kwenye ubongo wangu.”

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Jambo Tz